Header Ads

Mwimbaji Shakila Said Hatunaye Tena


Mwimbaji Shakila Said enzi za uhai wake.

Mwimbaji mkongwe wa muziki wa taarab nchini, Shakila Said amefariki dunia usiku huu baada ya kuanguka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbagala, Charambe jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mtoto wa mwisho wa marehemu aitwaye Shani ni kwamba marehemu amefariki baada ya kudondoka ghafla alipotoka kuswali. 

“Mama hakuwa mgonjwa hata kidogo, aliswali swala ya magharibi vizuri na baadaye akadondoka na kufariki,” alisema Shani huku akilia.
Marehemu Shakila ameacha familia ya watoto 13.

No comments