Header Ads

Mzee Akilimali achimba mkwara mzito ajabu


Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam
MWANACHAMA mkongwe wa Yanga ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, Ibrahim, Akilimali ‘Mzee Akilimali’ ambaye amekuwa katika mvutano na baadhi ya wanachama wenzake ametoa mkwara mzito juu ya wale wote wanaotishia maisha yake.
Akilimali alisema hayo jana baada ya kuhojiwa juu ya taarifa kuwa kuna baadhi ya wanachama wenzake wanataka kuvamia nyumbani kwake kutokana na kile ambacho imeonekana kama mzee huyo anataka kuwavuruga Wanayanga.
Akilimali ambaye amekuwa katika mvutano huo kutokana na awali kupinga wazo la Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, ambaye alitoa hoja ya kutaka kuikodisha timu hiyo, alishambuliwa kwa maneno na wanachama wenzake kuwa anachangia kuivuruga klabu hiyo kutokana na hoja zake tata za kumpinga Manji.
“Mimi nipo nyumbani kwangu na sijakimbia kwenda popote, kama kuna mtu ambaye ana mpango wa kuja kufanya fujo nyumbani kwangu aje ila ajue anajitakia mabaya.
“Mimi ndiyo nasema kama kuna mtu hataki uhai wake au hajitakii mema basi aje kufanya vurugu nyumbani kwangu,” alisema mzee huyo bila kufafanua.

No comments