Header Ads

Mzungu aliyefumwa akilawitiwa na vijana watatu ambapo habari za uhakika ni kwamba, ametimka nchin

Ama kweli Gazeti la Ijumaa Wikienda ni kiboko! Hii ni mara ya pili kwa muda wa mwezi mmoja, linaripoti habari na kuzaa matunda, mara ya kwanza ni ya Mbongo aliyeteswa na mwajiri wake Mchina, safari hii ni ya yule Mzungu aliyefumwa akilawitiwa na vijana watatu ambapo habari za uhakika ni kwamba, ametimka nchini.

TUANZE NA MZUNGU Katika gazeti hili, toleo la Jumatatu iliyopita, ukurasa wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa;

MZUNGU AFUMWA AKILAWITIWA NA VIJANA WATATU! Katika habari hiyo, Mzungu huyo alidaiwa kuwa ni raia wa Italia ambapo mapaparazi wa Wikienda , wakitumia kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’, walifanikiwa kumnasa mtasha huyo akiwa chumbani na vijana hao ambao walikuwa wakimfanyia kitendo hicho kwa ahadi ya malipo ya shilingi laki moja (100,000) kwa kila mmoja. Tukio hilo la kushangaza na aibu ya mwaka kwa mtu anayejitambua, lilijiri Agosti 4, mwaka huu, nyumbani kwa Mzungu huyo, Mikocheni jijini Dar.

BAADA YA WIKIENDA KUINGIA MTAANI Sasa, baada ya gazeti hili kusambaa mitaani Jumatatu iliyopita, habari mpya ni kwamba, Mzungu huyo ametimka nchini na kurudi kwako, kufuatia tukio lake kuanikwa.

CHANZO NI CHA KIPOLISI  Kwa mujibu wa chanzo cha kipolisi, baada tu ya habari zake kujulikana, ‘menejimenti’ (uongozi) ya kampuni ya ujenzi aliyokuwa akifanyia kazi yenye makao yake, Afrika Sana, Sinza, Dar ilimuweka chini na kumuuliza kuhusu habari hiyo ambapo Mzungu huyo
hakuwa na la kujibu zaidi ya kujiinamia.

 TWENDE NA CHANZO “Jamani mnajua yule Mzungu shoga ameikimbia nchi? Baada ya Gazeti la Wikienda kutoka na picha zake, uongozi wa kampuni aliyokuwa akifanyia kazi ulimuweka chini na kumuuliza kulikoni, jamaa akashindwa kujibu. “Uongozi ukamwambia kwa sababu hana la kusema ni vyema akaamua kuacha kazi. Sasa si unajua wenzetu weupe (Wazungu). Huwa hawana mjadala kwenye eneo la kuwajibika, Mzungu akasaini wino wa kuacha kazi.

” ASEPA USIKU WA MANANE “Kama hilo halitoshi, usiku wa saa nane akaondoka zake nchini kwa ndege kurudi kwao. Kama mnataka habari kamili nendeni pale kazini kwao,” kilisema chanzo hicho ambacho ni polisi.

WIKIENDA LATINGA OFISINI Juzi (Jumamosi), Wikienda lilifunga safari hadi ofisini kwa Mzungu huyo na kukutana na baadhi ya wafanyakazi ambao walisema viongozi hawakuwepo ofisini. Walipoulizwa kuhusu Mzungu huyo kuondoka nchini, walisema hawajui ila taarifa walizonazo ni kwamba, jamaa yupo mkoani Iringa kikazi na hajafika kazini hapo kwa muda wa siku saba.

WIKIENDA LAMRUDIA POLISI  Ilibidi Wikienda limrejee polisi aliyetoa ubuyu huo na kumweleza kuhusu madai ya Mzungu kwenda Iringa kikazi ambapo alisema: “Hamna, ameondoka zake yule bwana. Tena nataka kukwambia, alipoondoka alikabidhi mpaka gari. Uwanja wa ndege (wa Julius Nyerere, Dar es Salaam) alikwenda kwa kutumia teksi. “Hao wafanyakazi hawajui lolote. Mimi ndiye nakwambia hali halisi ilivyo, yule Mzungu ameondoka nchini, karudi
kwao.

” NYUMBANI KWA MZUNGU Jumamosi jioni, Wikienda lilifika nyumbani kwake Mikocheni na kukutana na mlinzi ambaye hakuwa tayari kujitambulisha ambapo alisema kuwa, zimekatika siku nne (tangu Agosti 9, mwaka huu) hajamuona Mzungu huyo nyumbani kwake. “Sijamwona Mzungu hapa nyumbani kama siku nne hivi. Ila siku alipoondoka alisema anasafiri lakini hakusema anakwenda wapi,” alisema mlinzi huyo.
 
 KWA NINI WIKIENDA KIBOKO? Tukirudi kwenye habari ya Mchina kudaiwa kumtesa Mbongo, Masanja Shokele, ni Wikienda hilihili liliandika habari hiyo kwenye toleo lake la Julai 25 hadi 30 ikiwa na kichwa;
 RAIS MAGUFULI HIVI NDIVYO MCHINA ALIVYOMTESA KIJANA HUYU BILA KUFANYWA CHOCHOTE.
 Katika habari hiyo iliyoshika kasi mitandaoni, Mchina mmoja ambaye jina lake halikujulikana, alidaiwa kumtesa Mbongo huyo kwa kumpa kipigo kwa madai kuwa, aliiba madini kwenye Mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro, Geita. Baada ya Wikienda kutoka, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba alilisoma gazeti hilo pendwa na kuamua kuchukua hatua kwa kwenda eneo la tukio kujionea mwenyewe ambapo alibaini ukweli na Mchina huyo ambaye awali hakuchukuliwa hatua yoyote, aliwekwa chini ya ulinzi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Baadhi ya wasomaji walilipongeza gazeti hili kwa kufichua uovu wa Mchina huyo wakisema kuwa, bila Wikienda, waziri asingejua na watenda maovu wangeendelea kuwepo wakitanua. “Jamani mimi nawapongeza sana Wikienda na magazeti mengine pendwa ya Global (Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi). Ninyi ni Voice of Voiceless (Sauti ya Wasio na Sauti).

No comments