Header Ads

Nani: Fergie alikuwa zaidi ya kochaVALENCIA, Hispania
KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Luis Nani amesema kocha wa zamani wa timu hiyo, Sir Alex Ferguson, ni kama baba yake kutokana na kile alichofanikiwa hadi sasa.

Nani alimaliza kipindi cha miaka nane kwenye kikosi cha United kwenye majira ya joto baada ya kujiunga Fenerbahce moja kwa moja baada ya kukaa kwenye timu hiyo kwa mkopo kwa msimu mmoja.

Kwa sasa mchezaji huyo ambaye yupo kwenye timu ya Valencia, amesema anaamini Ferguson amekuwa na msaada mkubwa kwenye mafanikio yake ya soka.

"United walinipa kila kitu ambacho ninacho kwa sasa kwenye soka. Namuona Fergie kama baba yangu, anaweza kukasirika lakini dakika moja baadaye anakuita na kukushika bengani anasema njoo hapa mwanangu.

“Lilikuwa jambo gumu kumuelewa mwanzoni kwa kuwa nilikuwa simfahamu lakini, nilipomtambua baadaye nilijua jinsi ya kukaa naye na kumuona kama baba yangu,” alisema Nani raia wa Ureno.

No comments