Header Ads

Njia rahisi za kupunguza unene

NI makala muhimu sana. Wastani wa maisha ya Mtanzania (na Waafrika wengi) hata wale waliosoma au wanaojiweza kiuchumi ni miaka 40-50.


 Kati ya sababu kuu zinazopunguza uhai wetu ni afya, unene na kutojua kujiangalia vyema afya zetu. 1-ULAJI Ipo mifumo miwili ya kula. Chakula unachokula na namna unavyokila. Unavyokula -Kuna kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini, vitamini, mafuta nk mara nyingi kwa siku; au kula milo michache (mmoja au miwili) mikubwa ili kujaza tumbo.

 Ulaji mdogo mdogo husaidia afya na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache. Tumbo lina musuli zinazofanya kazi kama mashine au mnyama. Gari likijaa sana hupata tabu kwenda. Punda hivyo hivyo. Ulaji mdogo mdogo unaosambazwa mara kadhaa kwa siku ni bora maana mwili unachambua kila kitu kwa wepesi na haraka. Unapokula milo michache mikubwa unapalilia zaidi mafuta mwili. 

PENDEKEZO LA KWANZA Asubuhi, kunywa maji kwanza, matunda, kisha ndiyo chai na vitu vingine kama mkate au maandazi). Wapo wanaodai kwamba wanakula matunda na mboga. Tatizo ni kwamba mipangilio yao huwa ya makosa. Mathalan wengi hula matunda baada ya chakula. 

Vimeng’enya chakula (enzymes) tumboni hufanya kazi namna tofauti. Mathalan vile vinavyonyambua matunda ni tofauti na vinavyomeng’enya vitu vigumu zaidi kama nyama au wanga.

 Matunda hunyambuliwa haraka zaidi kuliko vyakula vingine. Hivyo ni bora kula
matunda dakika 10-20 kabla ya chakula. Ukila baadaye matunda hugeuzwa aina fulani ya pombe (fermented food) inayoelea tu juu ya chakula na kubakia kitu kingine badala ya kuingizwa haraka ndani ya damu kupitia utumbo mdogo, wengu, moyo, ini, nk. Tatizo jingine ni kupika sana mboga hadi zikapoteza nguvu. -Mseto wa vyakula pia ni muhimu. Kwa mfano vyakula vyenye uchachu (acid) na vile vinavyomumunyuka haraka (alkaline) havitakiwi viliwe pamoja. Mfano ni matunda.


 Matunda chachu kama machungwa, mananasi na maembe yanatakiwa yawe pamoja; na yale laini zaidi: ndizi mbivu, matikiti maji, mapapai, matufaha, nk yaende kivyake, maana yana mfumo tofauti, wa kumeng’enywa. Hali hiyo pia iko katika nyama. Nyama nyeupe (ndege na samaki) tofauti na nyama nyekundu (ng’ombe, kondoo, nk) ziliwe tofauti. Chakula unachokula Watanzania/Waafrika hatuna tabia ya kula mboga mboga mbichi. Tunafuata ladha na mazoea kuliko thamani.

 Ulaji wa mboga mbichi ni upi? Ni mathalani ulaji wa salad. Tanzania tunaita kachumbari. Lakini si lazima iwe kachumbari ya nyanya, vitunguu na chumvi tu. Waweza kuchanganya matango, nyanya kwa maparachichi; au vitunguu saumu, giligilani na karoti. Huu mseto wa mboga mbichi ni mzuri ukienda na chakula chenye nyama za minofu na wanga (ugali, wali, ndizi za kupika nk). Ulaji wa wanga asubuhi, mchana na jioni kila siku huchangia sana katika unene.
 PENDEKEZO LA PILI Ugali kwa samaki; mboga ya majani ya matango kwa nyanya. Usiweke chumvi kwenye hiyo mboga mbichi ya majani. Itaendelea wiki ijayo

No comments