Header Ads

PAMOJA NA KUINGIA KIMYAKIMYA, BEJAIA WAPIGA MAZOEZI KWENYE UWANJA WANAOUTUMIA YANGA


 Ukitaka kuona watu wamepania, basi hii inaweza kuwa funzo. Maana inaelezwa kuwa kikosi cha Mo Bejaia kutoka nchini Algeria kimetua nchini kimyakimya.

Taarifa zimesema timu hiyo kutoka Algeria ambayo ipo Kundi A pamoja na Yanga, iko nchini bila ya kutoa taarifa kwa Yanga wala Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mo Bejaia inatarajia kuivaa Yanga katika mechi kama itashinda Jumamosi, itakuwa imejihakikishia kucheza hatua ya nusu fainali kwa asilimia 90.

Hivyo, Waarabu hao wa Algeria wametua nchini kimyakimya huku Yanga wakitarajia kuwa watafika kesho au keshokutwa.


No comments