Header Ads

Picha chafu zatibua penzi la Masogange 18+
Picha chafu z i l i z o v u j a zikimuonesha Video Queen wa Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ akiwa kihasarahasara na mwanaume anayesemekana ni msanii wa Bongo Fleva, Regnald Raymond ‘Reggy’ zimeibua hasira kwa mpenzi wake ambaye ni mwigizaji wa Bongo Muvi, Rammy Galis na kutishia kuvunja penzi lao.

 Chanzo chetu makini kabisa kilisema kuwa ingawaje inadaiwa kuwa picha hizo ni moja ya kurekodi nyimbo inayoitwa Kampa Kampa Tena ya mwanamuziki huyo lakini baadhi ya picha zilizovuja ni chafu na haziko kwenye video ya wimbo huo kitu ambacho kilizidi kuwapa maswali watu mbalimbali ya kuwa kuna kitu kingine zaidi ya picha hizo.

 “Sawa wao wenyewe wanasema kuwa ni vipande vya picha vilivyopo kwenye video ya nyimbo hiyo lakini kwenye nyimbo hiyo ukiitazama vipande hivyo havionekani kabisa,” kilidai chanzo hicho. Mpashaji wetu huyo aliendelea kufunguka kuwa baada ya picha hizo kuvuja mpenzi wa sasa wa Masogange inadaiwa alimpigia simu kijana huyo na kumpa kashikashi huku
akimtaka aache kusambaza picha hizo la sivyo wasije kulaumiana.

Gazeti hili lilipoinyaka habari hiyo lilimtafuta kwanza mwanamuziki huyo ambapo alikana kuwa yeye si mwanzilishi wa kusambaza picha hizo kwa sababu hakuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Rammy Galis alipotafutwa kuzungumzia jinsi picha hizo zilivyomchefua hakuweza kupatikana mara moja. Hata hivyo, Masogange alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi alisema: “Unajua kila kukicha watu wanapenda kuibua mambo, ile ni video na mpenzi wangu anaijua, kama kuna kutofautiana na mpenzi wangu picha hizo wala siyo sababu.”

HABARI NA GAZETI LA IJUMAA

No comments