Header Ads

Pogba: Tulieni, nipo fiti kwa kaziMANCHESTER, England   
STAA wa Manchester United, Paul Pogba amesema atakuwa fiti kucheza leo Ijumaa wakati Manchester United itakapovaana na Southampton katika mechi ya Premier League kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Mchezo ni wa pili katika ligi hiyo baada ya ule wa kwanza United kushinda mabai 3-1 dhidi ya dhidi ya Bournemouth.

Pogba, mchezaji ghali zaidi duniani hakucheza mchezo wa kwanza kutokana na kuwa na adhabu ambayo aliipata nchini Italia wakati anaichezea Juventus.

Hata hivyo, inaamika kuwa Kocha Jose Mourinho atamtumia kwenye mchezo wa leo ambao unaonekana kuwa mkali kwa timu zote.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 23, anatarajiwa kupokewa kwa furaha kubwa na mashabiki kama atacheza kutokana na kiwango ambacho amekuwa akikionyesha msimu uliopita alipokuwa Juventus.

"Nafikiri kama ni suala la kucheza basi aulizwe kocha kwa kuwa ndiye anayejua kikosi chake.

“Nimefanya mazoezi na timu kwa siku kumi hivyo nipo fiti kwa asilimia 100 kuweza kutumika kwenye kikosi cha United.

"Nipo tayari kufanya jambo lolote kwa United, nipo fiti sana kwa upande wangu lakini kocha anaweza kuwa anajua zaidi.

"Ninafuraha kucheza soka, nia yangu ni kuhakikisha kila siku nakuwa fiti, nataka kuwa namba moja na kuwa bora.

“Nia ya timu kwanza ni kutwaa ubingwa wa England, lakini pia tunataka kurudi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya sehemu ambayo timu hii imezoea kuwepo.

“Naamini kuwa tunaweza kufanya vizuri, kila mmoja hapa ana nia na morali ya hali ya juu ya kufanya vizuri,” alisema Pogba.

No comments