Header Ads

Rio Olympic: Fursa kwa Vijana, Watembea Wakiuza Kondom Mitaani


Rio, Brazil
WANAMICHEZO wengi walioko Rio nchini Brazil kwa ajili ya michuano ya 2016 Rio Olympics wameonekana kufanya vitu tofauti sana mwaka huu ili kuwawezesha kila mmoja kupata kile anachokidhamiria kwenye mashindano hayo. Kila mmoja yuko ‘bize’ kujituma ili ahakikishe angalau anapata medali kama ilivyo kawaida kwa tuzo za mashindano hayo.
Matukio mengi yameripotiwa kutokea huko Rio, lakini kuna hili la njemba mmoja aliyejulikana kwa jina la Eric, yeye na vijana wenzake wamekuwa wakitembea na mifuko ya kondomu mitaani huku wakihamasisha ngono salama kwa wanamichezo hao.
Wamekuwa wakionekana kwenye maeneo tofauti katika Jiji la Rio huku wakiuza kondomu hizo tena hadharani kama machinga anavyotembeza vyombo na nguo mtaani tena bila aibu. Hii imeonekana kuwa fursa kwa vijana hao kwenye mashindano kwa kuwa kuna wageni wengi ambao wanatumia zana hiyo.
Baada ya kuhojiwa na wanahabari wa E! News, Eric amejibu haya; “Mimi sioni aibu kuuza kondomu hadharani kwa maana ni biashara inayoniingizia kipato…. kuna baadhi ya wanamichezo hawafanyi kabisa ngono wakiwa kwenye mashindano makubwa kama haya, lakini kuna wengine wanaamini bila kufanya ngono hawawezi kufanya vizuri kwenye michezo yao na kupata tuzo, hao ndiyo wateja wangu haswa, ” alisema Eric.
“Kondomu pia inasaidia kujikinga na maambukizi ya virusi vya zika ambavyo kwa sasa ni tishio hapa Brazil, kwa hiyo naamini ninachokifanya siyo kosa bali nina jali afya za wanamichezo.” Alimalizia Eric.
And thus, we thank Eric and his colleagues for their service!

No comments