• Latest News

  August 19, 2016

  Sadio Mane aumia, kukikosa Burnley  LIVERPOOL, England
  MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Sadio Mane anaweza kushindwa kucheza mchezo wa kesho dhidi ya Burnley.

  Mchezaji huyo ambaye alionyesha kiwango kizuri kwenye mchezo dhidi ya Arsenal, wikiendi iliyopita, anatarajiwa kukosa mchezo huo baada ya vipimo kuonyesha kuwa ana matatizo ya misuli ya bega.

  Mane alipelekwa hospitalini kutazamwa bega baada ya kuumia kwenye mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Melwood.

  Hata hivyo, vipimo vimeonyesha kuwa mchezaji huyo ameumia mfupa wa bega lakini halijachomoka hali ambayo ilimpa ahueni Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp.

  Taarifa zinasema ataendelea kuangaliwa na madaktari wa timu hiyo na ana asilimia ndogo ya kucheza mechi dhidi ya Burnley.

  Mane ambaye alifunga bao moja Jumapili iliyopita kwenye ushindi wa timu yake dhidi ya Arsenal alijiunga na Liverpool akitokea Southampton kwa pauni milioni 30.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Sadio Mane aumia, kukikosa Burnley Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top