Header Ads

SAMATTA AENDELEA KUFUNIKA UBELGIJI APIGA BAO DAKIKA YA 90 NA KUIBEBA GENKMshambuliaji Mtanzania Mbwana Samatta amezidi kuonyesha makali yake nchini Ubelgiji baada ya kuifungia KRC Genk bao muhimu lililoipa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Oostende.

Karelis ndiye alikuwa wa kwanza kufunga upande wa Genk, ilikuwa ni katika dakika ya 50, Samatta akaongeza katika dakika ya 90+1, yaani katika ile dakika moja ya nyongeza.

Bao hilo la Samatta limekuwa lililoibeba Genk kwa kuwa, Musona aliifungia Oostende bao dakika 90+3 ikiwa ni ya mwisho kabisa baada ya kuongezwa dakika tatu.

Kama ingekuwa bado wanaongoza kwa bao moja la Karelis, maana yake Genk wangeambulia sare ya bao 1-1 baada ya dakika 90.

No comments