• Latest News

  August 09, 2016

  Shilole ‘awaka’ kisa kutoka na Jay Moe

  Stori: Leonard Msigwa
  MREMBO ambaye jina lake liko juu kwa sasa kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ hivi karibuni amewaka baada ya kubanwa maswali juu ya tetesi za uhusiano wake na Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’.
  Akistorisha na Uwazi Showbiz, Shilole alifunguka kuwa hana uhusiano na mkali huyo wa ngoma ya Pesa Madafu na hajawahi kufikiria kutoka naye na anawashangaa watu wanaomhusisha kuwa kwenye mahaba na Jay Moe.
  Jay-MoeJay Moe.
  “Watu bwana wanashindwa kufuata yao wanakalia kuchonga yawenzao, mimi Jay Moe ni kaka yangu, tumeshibana na hatuna uhusiano wowote,” alisema Shilole.
  Kwa upande wa Jay Moe amefunguka kupitia kwenye mitandao ya kijamii juu ya kuzisikia tetesi za yeye kutoka kimapenzi na Shilole, amedai pia hazina ukweli wowote maana mwanadada huyo ni mshikaji wake wa karibu tu!
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Shilole ‘awaka’ kisa kutoka na Jay Moe Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top