Header Ads

SNURA ATESWA NA NDOTO ZA MAPENZI


 Staa wa Wimbo wa Chura, Snura Mushi.
 Staa wa Wimbo wa Chura, Snura Mushi anadaiwa kuteswa na ndoto za kimapenzi huku ikielezwa kuwa, mara kadhaa amekuwa akisimulia jinsi anavyotokewa ndotoni na msanii mkubwa wa Bongo Fleva. Rafiki wa karibu wa msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina alilitonya gazeti hili kuwa, Snura kila siku amekuwa akieleza kuwa, anatokewa na msanii huyo kwenye ndoto na kujikuta wakiingia kwenye mahaba mazito.

 “Mwenyewe anaeleza kuwa, anahisi anampenda sana ndiyo maana anaota akiwa naye mara kibao. Halafu sasa alivyodata kila akimuota eti akikurupuka anatafuta ilipo picha yake na msanii huyo kisha kuikumbatia, yaani ana wakati mgumu sana. “Mimi nimemwambia amtokee huyo msanii amwambie ukweli kuwa anampenda lakini anadai eti akifanya hivyo anahisi atakuwa amejitongozesha na mbaya zaidi msanii huyo anaweza akawa na mtu wake,” alisema mtoa ubuyu huyo na kuongeza: “Kanitajia jina la msanii huyo mkubwa tu hapa Bongo lakini sasa nikiwatajia nitakuwa sijafanya poa, ninyi kama vipi mtafuteni mwenyewe, kama ataona freshi kufunguka gazetini, afanye hivyo.”

 HUYU HAPA SNURA
 Baada ya kunyetishiwa habari hiyo, mwandishi wetu alifanya jitihada za kumpata Snura na alipopatikana alikiri kufa na kuoza kwa msanii huyo ambaye hakumtaja ‘streiti’ ila akataja majina manne na kudai kuwa ni mmoja kati ya hao. “Labda niwatajie majina manne, mmoja kati yao ndiye anayeutesa moyo wangu. 

Kiukweli ananifanya namuwaze kila wakati, huwezi amini sasa hivi naimba nyimbo zake, napenda kuangalia picha yake kila wakati, nahisi hata kushindwa kufanya kazi kwa sababu yake,” alisema Snura. Snura aliwataja wanamuziki hao kuwa ni Izzo Biznes, Raymond, Ali Kiba na Man Fongo ambapo mwisho alidai kuwa kuna siku atampa ukweli na endapo atamkubalia, atampetipeti kuliko kawaida kwani hajawahi kupenda kiasi alichompenda

No comments