• Latest News

  August 25, 2016

  Suarez aanza kwa kumsifia Messi

  BARCELONA, Hispania
  MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Luis Suarez amesema kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Lionel Messi ameanza msimu huu kwa kasi kubwa sana. Barcelona walianza msimu wa ligi kwa kuibuka na ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya Real Betis wikiendi iliyopita.
   
   Messi alikuwa na kipindi kigumu hapo nyuma na timu yake ya taifa ya Argentina baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Copa Amerika hali iliyomfanya atangaze kustaafu kuichezea nchi hiyo. 

  Lakini kitendo cha kuifungia Barcelona mabao mawili kwenye mchezo huo wa kwanza na kutoa pasi kwa Suarez kimemfanya mchezaji huyo kuamiani kuwa msimu huu utakuwa wa staa huyo wa Argentina. 

  “Leo ameanza kwa kasi kubwa sana, hakika huyu ni mchezaji bora duniani, kila mmoja hapa anafurahia kuona kasi yake,” alisema Suarez na kuongeza kuwa: “Uwezo tuliouonyesha unadhihirisha tunautaka ubingwa wa Hispania msimu huu, hakika hakuna anayeweza kutuzuia sana, sisi ni kati ya wale wanaopewa nafasi ya kufanya vizuri. “Tumeanza vizuri na hali hii inatupa nguvu ya kuamini tunaweza kufanya vizuri msimu huu, ni jambo la k
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Suarez aanza kwa kumsifia Messi Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top