• Latest News

  August 31, 2016

  Taarifa Toka IKULU : Rais Magufuli atengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Agosti, 2016 amemteua Bw. Doto M. James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

  Kabla ya uteuzi huo Bw. Doto M. James alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera).

  Bw. Doto M. James ataapishwa kesho tarehe 01 Septemba, 2016 saa 2:45 Asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Kufuatia uteuzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile atapangiwa kazi nyingine.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es Salaam
  31 Agosti, 2016
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Taarifa Toka IKULU : Rais Magufuli atengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top