Header Ads

Toyota Chaser Yaligonga Passo Lililopaki Bamaga-Mwenge


 Mmiliki wa gari lililogongwa aliyejitambulisha kwa jina la Dalia Ahmed (kulia mwenye sketi ya pinki) akiwa na trafiki kwenye ajali hiyo
Trafiki anayedaiwa kumfukuza aliyesababisha ajali hiyo akipata maoni ya baadhi ya mashuhuda.

TOYOTA Chaser lenye namba za usajili T 817 AFK ambaye mmiliki wake hakutambulika, limeligonga gari lingine lililokuwa limepaki lenye namba za usajili T949 CGS  linalomilikiwa na Dalia Ahmed katika barabara inayopita mbele ya Ofisi za Kampuni ya Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mtandao huu umenasa baadhi ya picha zinazoonesha tukio hilo leo (Agosti 30) kabla ya kuondolewa na mmiliki wa gari lililogongwa.
Akizungumza mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Rehema, alisema kuwa gari lililosababisha ajali lilikuwa likitokea katika barabara ya Sinza Afrika-Sana likipita barabara inayotokea Hospitali ya Marie Stopes na dereva alipofika karibu na ofisi za Global, gari lake likiwa kasi aliingia uchochoroni  na kuligonga gari lililokuwa limepaki.
Mwandishi wetu alipotaka kupata maelezo juu ya ajali hiyo kutoka kwa trafiki anayedaiwa alikuwa akimfukuza mwenye gari lililosababisha ajali, alisema kuwa yeye siyo msemaji hivyo mwandishi akitaka maelezo aende kituo cha polisi cha Oyster Bay ambapo ndiko magari hayo yalitakiwa kupelekwa.

No comments