• Latest News

  August 29, 2016

  Ufafanuzi wa CHADEMA kuhusu taarifa ya kuahirishwa Operesheni UKUTA


  CHADEMA inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu andiko linalosambazwa mitandaoni likimnukuu Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe kuwa ameahirisha Operesheni UKUTA na maandalizi ya Septemba 1.

  Tunaomba umma upate taarifa sahihi kuwa Mwenyekiti Mbowe hajafanya mkutano na waandishi wa habari mahali popote pale kuzungumzia kuahirisha Operesheni UKUTA inayoendela nchi nzima wala kuzuia maandalizi ya Septemba 1.

  Kupitia taarifa hii, chama kinawataka viongozi, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA na Watanzania wote wazalendo na wapenda haki, kupuuza andiko linalosambazwa mitandaoni .

  Msisitizo unaendelea kutolewa kuwa Operesheni UKUTA ambayo imelenga kusimamia utawala unaoheshimu Katiba ya Nchi na kulinda sheria na maandalizi yanaendelea nchi nzima.

  Imetolewa na;

  Tumaini Makene
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
  CHADEMA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Ufafanuzi wa CHADEMA kuhusu taarifa ya kuahirishwa Operesheni UKUTA Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top