Header Ads

Upinzani Waongoza Kura za Urais Zambia

Hakainde-Hichilema-And-His-Riches-–-Companies-Owned-By-HH-That-You-Didn’t-KnowHakainde Hichilema
TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini Zambia (ECZ) imetangaza matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu uliofanyika juzi Alhamisi ambayo yanaonesha kuwa mgombea urais wa chama kikuu cha upinzani nchini humo, United Party for National Development (UPND), Hakainde Hichilema, anaongoza kwa kura 47, 706 akifuatiwa na rais wa sasa wa nchi hiyo, Edgar Lungu mwenye kura 41, 572.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa Hichilema mwenye asilimia 57.55 yuko mpele ya Edgar Lungu kwa kura zaidi ya elfu sita kwenye majimbo 8 kati ya 156 ambayo yamekwisha hesabiwa.
zambiaTume ya Uchaguzi ya Zambia ilipinga shutuma kutoka kwa Bw Hichilema kwamba ilikula njama na serikali ya kuchelewesha kutangaza matokeo ya uchaguzi.
Ilisema ushiriki wa wapiga kura zaidi ya asilimia hamsina na saba unamaanisha kwamba shughuli ya kuhesabu kura itachukua muda kuliko ilivyo tarajiwa.
zambiaaEdgar Lungu alichaguliwa mwaka jana kwa ushindi mdogo kufuatia kifo cha rais aliekuwepo mamlakani wakati huo, Michael Sata.
Mgombea wa The United National Independence Party (UNIP), Tilyenji Kaunda anashika nafasi ya tatu akiwa na kura 541 akiifuatiwa na mgombea wa PAC mwenye kura 527.
Jumla ya wapiga kura walioandikishwa ni 163, 520 na waliopiga kura ni 94, 100. Wakati kura zilizoharibika ni 2,567.

No comments