Header Ads

VIERA: POGBA atabaki kuwa Pogba tu

MCHEZAJI wa zamani wa Manchester City na Arsenal, Patrick Vieira, amemwambia kiungo Paul Pogba kuwa hawezi kuwa Cristiano Ronaldo wala Lionel Messi. Pogba amejiunga na Manchester United msimu huu akitokea kwenye kikosi cha Juventus cha Italia akiwa ndiye mchezaji anayeshikilia rekodi ya kusajiliwa ghali zaidi duniani kwa sasa. 
 
Awali mchezaji huyo baada ya kutua kwenye kikosi cha United alikuwa akielezwa kuwa ni kama Vieira mpya kwenye soka, lakini Mfaransa mwenzake huyo amemwambia aachane na kutumia majina ya watu. 

“Mimi ni shabiki mkubwa sana wa Pogba, nafikiri huyu  ni mchezaji bora duniani kwa sasa,” alisema Vieira ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya New York City FC. “Hakuna ambaye anaweza kubisha kuhusu ubora wa Pogba lakini kila mara nimekuwa nikiamiani kuwa Ligi Kuu England ni ngumu na bora kuliko nyingine zote duniani, lazima hapa atakuwa na presha kubwa. 

“Nilisoma kitu ambacho kilisemwa na Jose Mourinho kuwa Pogba atakuwa sawa na Lionel Messi au Cristiano Ronaldo. “Hawezi kuwa hivyo, nafikiri Pogba atabaki kuwa yeye na Ronaldo atakuwa Ronaldo. “Kama watu wanafikiri anaweza kufunga mabao 40 kama Ronaldo hiyo ni ishu nyingine, lakini atakuwa tofauti na Ronaldo kwenye muonekano pamoja na mawazo, nafikiri ni vizuri akakubali kuwa yeye na siyo mtu mwingine,” alisema Vieira ambaye pia aliwika akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa.

No comments