Header Ads

Vodacom Yawasogelea Wafanyabiashara Wadogo

1
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Kaijage (katikati), akibonyeza kitufe kwenye laptop kama ishara ya uzinduzi wa huduma hiyo.
2
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,  Ian Ferrao, akizungumza jambo kwenye uzinduzi huo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
3
Mshereheshaji wa shughuli hiyo, Ephraim Kibonde, akiwajibika.
4
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Kaijage, akiongea jambo mbele ya waalikwa wa shughuli hiyo.
KAMPUNI ya mtandao wa simu za mkononi Vodacom, leo imewasogelea wafanyabiashara wadogo baada ya kuzindua huduma ya Uhusiano wa wafanyabiashara wadogowadogo na wa kati, uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro, jijini Dar es Salaa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Kaijage kuwa mgeni rasmi.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Waziri Kaijage alisema Vodacom imeanzisha jambo linalopaswa kuigwa, hasa kipindi hiki ambacho serikali ikiwa katika harakati za kukuza uchumi wa nchi, ikipigana kwa hali na mali kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati.

“Nimefurahi sana Vodacom kunialika  kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huu ambao kwa namna moja au nyingine wamenileta kuzungumza na walengwa wangu, maana uchumi siku zote huanzia chini kwenda juu, nawaomba kampuni zingine zianzishe mpango huu ili tuweze kuisukuma nchi kwa pamoja kuifikisha kwenye uchumi wa kati na unaoendelea,” alisema Kaijage.
(PICHA/HABARI: MUSA MATEJA/GPL)

No comments