Header Ads

WASHINDI WA TECNO C9 CHALLENGE WAPATIKANA

Edward Josephat, mshindi wa kwanza wa C9 Challenge baada ya kukabidhiwa zawadi yake. ‪#‎SeeLifeInC9‬
Instagram : @eddiephotography93


Baada ya wiki kadhaa tangu Tecno Mobile Tanzania izindue shindano la C9, hatimaye shindano hilo limefikia mwisho na washindi wa kwanza na wa pili wametangazwa na kampuni hiyo. Washindi hao ni Edward Ruthaihwa na Michael Nyantori ila mpaka sasa taarifa tulizpokea ni za Edward na tuna picha zikionyesha akipokea zawadi hiyo, tutaendelea kukuletea habari kadri tunavyozipokea. Haya ndio yaliyojiri wiki hii. 
Pichani ni Mmoja wa Wakilishi wa Tecno (kushoto) na kulia ni mshindi Edward akikabidhiwa zawadi yake ya Camon C9 mpya ndani ya box.
Pichani ni Edward baada ya kukabidhiwa Camon C9 akiwa na hamu kubwa ya kufungua simu hiyo ili aweze kujivunia ushindi wake.
Ili kushinda, Edward aliweza kukamilisha challenge zifuatazo;
  • Piga picha kuonesha anga la Tanzania
  • Piga picha kuonesha maisha ya kila siku ya Tanzania
  • Piga picha kuonesha mazingira ya Tanzania nyakati za usiku
  • Piga picha za kuonesha usafiri unaotumika Tanzania
  • Piga picha ukionesha watu wa jamii ya Kitanzania
. Handle yake ya Instagram ni @eddiephotography93 unaweza kutizama picha zaidi
Facebook: https://www.facebook.com/TECNOMobileTanzania
Instagram: https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/No comments