Header Ads

WATANZANIA WANAZIDI KUNG’AA NA TECNO, SHINDANO LA KUJISHINDIA CAMON C9 LINAENDELEA


Tecno Mobile Tanzania ilizindua shindano la kipekee siku chache zilizopita na mapokezi yamekuwa mazuri kutoka kwa watu huku tukiona washiriki mbali mbali wakishindania zawadi itakayotolewa ya simu kali ya Camon C9. Simu hiyo yenye sifa na uwezo wa kufanya mambo mengi ikiwemo “Make-up Feature” ambayo inarahisisha na kuwezesha upakaji wa make-up kidijitali, uwezo wa kujumuisha watu wengi zaidi kwenye picha moja, camera yake imepewa jina la Camera ya Mwendokasi kutokana na uwezo wa kukamata matukio hapo kwa papo yaani “High Speed Focus”, kuna mengi ndani ya simu hii na imesababisha iwe gumzo au kwa kisasa wanasema “Talk of the town”.                                                                                        
Mbali na uwezo huo wa hali ya juu katika kupiga picha, Camon C9 pia ina nafasi ya simcard mbili ambazo zote zina uwezo mtandao wa 4G LTE utakaokuwezesha kupandisha picha zako mtandao kwa kasi zaidi. Pia simu hii ina mashine yenye uwezo wa kufanya kazi kwa haraka zaidi hivyo kufanya utumiaji wa application mbalimbali kuwa rahisi zaidi.

Simu ina uwezo wa kupiga picha kutumia sauti (Voice command) ama ishara za vidole (Gestures)  hivyo basi kukuwezesha kupiga picha bila kuishika simu.

MUDA WA SHINDANO LA TECNO C9 CHALENGE KUONGEZWA

Kwa sababu ya idadi ya washiriki kuhitaji nyongeza ya muda ili kuwewawezesha kukamilisha challenge zote, kampuni ya simu ya Tecno imeongeza muda hadi Jumatano 3 Agosti 2016 kuwezesha washiriki zaidi kujiunga


Challenge kadha zimetawala wiki iliyopita na shindano bado linaendelea ambapo tumeona watu wengi wakishiriki kwa kuweka picha katika mitandao yote ya kijamii kuanzia Facebook, Twitter na Instagram, unaweza kujionea mwenye kwa ku search #SeeLifeInC9.  Endelea kushiriki challenge hizi na uwe katika nafasi kubwa ya kushiriki na kuibuka mshindi.

Ili kushinda, inabidi ushiriki challenge zifuatazo

·       Piga Picha ukiwa kwenye mnara wowote wa Askari au mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.
·       Piga picha ya Panorama ikionesha eneo kubwa au vitu vingi
·       Piga picha ukiwa umeruka angani (Picha haitakiwi kuonesha umegusa ardhi au kukanyaga kitu chochote)
·       Piga picha kuonesha uoto wa asili wa Tanzania
·       Piga picha kuonesha anga la Tanzania
·       Piga picha kuonesha maisha ya kila siku ya Tanzania
·       Piga picha kuonesha mazingira ya Tanzania nyakati za usiku
·       Piga picha za kuonesha usafiri unaotumika Tanzania
·       Piga picha ukionesha watu wa jamii ya Kitanzania​
Ili kushinda hakikisha unafanya “challenge” angalau 5 na unapoweka picha kwenye mitandao ya Facebook, Twitter na Instagram hakikisha unatumia hashtag hizi #SeeLifeinC9 na #TecnoCamonC9 na tag Tecno Tanzania. Washindi watapatikana kwa idadi ya Likes, Retweets na Shares. Fuata Tecno Mobile kwenye mitandao ya kijamii kujua zaidi

Facebook: https://www.facebook.com/TECNOMobileTanzania/?fref=ts

Instagram: https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/

Twitter: https://twitter.com/TECNOMobileTZ

No comments