Header Ads

Wema Sepetu Aumbuka! Licha ya Kukana Kutumia Mkorogo..Pich Yake Ya 2007 Yafichua siri zipo hapa


  Staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.

Mara kadhaa staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amekuwa akitumia nguvu kubwa kukanusha kwamba mabadilko ya mwili wake hayana uhusiano na utumiaji wa mkorogo lakini safari hii mwanadada huyo ameumbuka baada ya picha yake aliyopigwa mwaka 2007 kunaswa. 

SKENDO YA KUTUMIA MKOROGO 
Wema amekuwa akitafunwa na skendo ya kutumia vipodozi vikali ‘mkorogo’ katika kutaka kubadili muonekano wa ngozi yake ambapo katika siku za hivi karibuni sehemu kubwa za mwili wake zinaonekana kuharibika. Maeneo ya mwili wa msanii huyo yanayoonekana wazi kuathiriwa na matumizi ya vipodozi vikali ni pamoja na mikononi, kifuani, miguu na hasa mapajani ambapo baadhi ya mashabiki wake kuna wakati walifikia hatua ya kumuambia ukweli kwamba, mikorogo anayotumia inamharibu. 
 
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ wa sasa anadaiwa kutumia mkorogo.

“Wema namjua vizuri, ile siyo ngozi yake kabisa. Ninavyojua alikuwa na ‘kangozi f’lani ameizing’ lakini alipoamua kutumia mkorogo ndipo akajiharibu. “Ningekuwa na uwezo wa kuongea naye uso kwa uso ningemwambia anajizeesha wakati bado ni mrembo,” alisema shabiki mmoja wa msanii huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mwanaheri wa Sinza jijini Dar. 

SKENDO YA KUONGEZA MAKALIO 
Mbali na madai ya mwananada huyo kutumia mkorogo, pia amekuwa akiingizwa kwenye orodha ya mastaa wa kike Bongo ambao wameongeza ukubwa wa makalio yao kwa kutumia dawa za Kichina. 

 

 Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ enzi za zamani.
ADAI YUKO ‘OG’ Kufuatia madai kuwa anatumia mkorogo na kwamba hata shepu yake ni ya dukani, Wema alinukuliwa na gazeti hili akikanusha madai hayo huku akieleza kuwa, yeye ni orijino ‘OG’ na wanaodai anajichubua, hawamjui vizuri.

 MAMA YAKE NAYE AMTETEA Hivi
 karibuni mama wa msanii huyo, Miriam Sepetu ‘Mzaa Chema’ naye alivunja ukimya na kueleza kuwa, mwanaye anasingizwa mambo yasiyo na ukweli kwani anachojua yeye hatumii mkorogo wala dawa za kuongeza makalio. “Nawashangaa wanaomsema vibaya mwanangu kuwa amejaladia (wowowo), wengine wanasema anatumia dawa za Kichina, mara mkorogo, hakuna ukweli
wowote kwani Wema ni mwanangu, namjua alivyo. Hakuna kitu alichoongeza kwenye mwili wake,” alisema mama Wema.


 PICHA YA 2007 YAMUUMBUA 
Katika kupekuapekua kwenye makabrasha ya Ijumaa, hivi karibuni ilinaswa picha ya Wema aliyopigwa mwaka 2007, mwaka mmoja baada ya kuibuka Miss Tanzania 2006 ambapo anaonekana akiwa na ngozi ‘nechuro’, tofauti na aliyo nayo sasa. Katika picha hiyo ambayo inamuonesha akiwa ‘kisu’ ile mbaya, mwili wake unaonekana ukiwa na rangi tofauti na alivyo sasa, mazingira yaliyoonesha wazi kuwa, ametumia mkorogo uliosababisha sehemu za mwili wake kuharibika. Aidha, katika picha hiyo ambayo inaonekana alikuwa kwenye mtoko wa usiku, Wema anaonekana akiwa na nywele zake ndefu halisi tofauti na sasa anavyotumia mawigi, kope na nyusi zake ni za asili wakati sasa ni fulu kujichora mawanja, kucha zake ni ‘nechero’ na sasa makucha marefu ya dukani yanahusika.
 

AMEKOMALIA UREMBO WA DUKANI? 
Hata hivyo, katika uchunguzi wa kawaida uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, Wema alikuwa binti mwenye urembo wa asili na hicho ndicho kilichomfanya ashinde Taji la Miss Tanzania mwaka 2006 lakini kadiri siku zilivyokwenda, alianza kuukataa uhalisia wake na kuusaka urembo wa dukani, hali iliyomfanya awe na muonekano alionao hivi sasa. 

MWENYEWE ANASEMAJE? 
Mwandishi wetu alimtafuta Wema ili kuuzungumzia tena muonekano wake wa sasa akilinganisha na anavyoonekana kwenye picha hiyo ya mwaka 2007 lakini jitihada hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea. 

TUJIKUMBUSHE
 Mwaka 2013, Wema alikwenda nchini China na ikadaiwa kuwa akiwa huko alitumia kiasi cha shilingi milioni 13 kwa ajili ya kubadili muonekano wa ngozi yake baada ya watu kumuandana na kusema alikuwa ameharibika.

No comments