• Latest News

  August 30, 2016

  Wema Sepetu: Sirudi Tena Dar kwa sasa nipo mkoani Arusha

  Malkia wa filamu Wema Sepetu amelikimbia jiji la Dar es salaam na kuamua kuanzisha makazi mapya mkoani Arusha kama alivyodai mwenyewe.

  Mwigizaji huyo ambaye kwa sasa yupo mkoani Arusha ameonyeshwa kuvutiwa na jiji la Arusha na kuamua kuwarusha roho mashabiki wake kwa kuwaambia kwamba hatarudi tena Dar es salaam.

  “My shouger nikimpenda hovyooo, kweli watu tumetoka mbali, huyu ndiye atakayenifanya nihamie Arusha kwakweli,” aliandika Wema katika picha hiyo hapo juu akiwa na rafiki yake.

  Kadhi siku zinavyozidi kwenda mrembo huyo anaonyesha kuendelea kuvutiwa mji wa Arusha.

  “Nirudie nini Dar mie, kurudi Dar majaliwa, na sirudi Dar ng’o,” aliandika Wema katika ujumbe wake wa pili.

  Hata hivyo uwamuzi huyo umepokewa tofauti na baadhi ya mashabiki wake katika mitandao ya kijamii.

  Haya ni maoni ya baadhi ya mashabiki wake.

  Hopeolivier24
  Dar bila Wema Itawezekana kweli? Itakuwa manispaa maana jiji unaliamishia Arusha๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

  Zai_miss
  Kwaiyo ushahamia arusha jamani khaaaa vigoma vyako itakuwaje My mmmh ila umefanya lamaana maana bongo kwa moto arusha Baridi kishezi๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

  Theonerealdully
  Utarudi tuu. Watu wa dar miji mingine hamuiwezi hekaheka zenu na mafoleni mwayapenda hivyohivyo

  Andymsalali
  jamn kwann, rudi bhana, tumekuzoea wenyew kukuona dar

  Zeyaabdallah
  Wema Rudi home coz matatizo hayakimbiwi dadaangu mpenz Wang.sawa Bali unatakiwa uyakabi

  Bongo5
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Wema Sepetu: Sirudi Tena Dar kwa sasa nipo mkoani Arusha Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top