Header Ads

Wifi unapomsakama mwanamke mwenzako unashangaza!

NIANZE kwa kumshukuru Mola ambaye ni mwingi wa rehema kwa kutufikisha Jumatatu nyingine njema sana. Nawe msomaji wangu wa XXLove asante kwa kuunga mkono safu hii na kujipatia nakala yako kila Jumatatu bila kukosa. Wiki hii makala haya yatawaangazia mawifi ambao wamekuwa wakiwasimanga au kuwasakama wanawake walioolewa na kaka zao yaani mawifi na kusahau kuwa hata wao ni wanawake na wataolewa kisha watakutana na mawifi pia kama walivyo wenzao.


 Utafiti wa safu hii umebaini kwamba, kama kuna watu ambao huwa wana maneno ya shombo chini ya jua, basi mawifi wanaongoza (mimi nawaita shemeji). Sijui huwa wamechanjiwa au inakuwaje! Cha ajabu wifi huyohuyo aliyekuwa akimzodoa mke wa kaka yake, kwa kumkejeli na maneno machafu kama, ‘wifi wa miye utakuwa wewe? Nahisi kaka yangu alikosea kukuoa na kwa taarifa yako nitakukomesha hadi utuachie kaka yetu’.

 Amini usiamini kuwa leo hii huyohuyo aliyemwambia mwenzake hafai kuwa wifi yake, naye anapata mume na analalamika kutendewa vibaya na wifi yake! Yeye amesahau alivyokuwa akimsimanga na kumnyanyasa mke wa kaka yake bila sababu yoyote ya msingi. Kiukweli, wanawake (mawifi) wa sampuli hii huwa mnasikitisha na kushangaza sana. Kwa nini mnakuwa na gubu kiasi hicho? Kwa nini hampendani? Kwa tabia hiyo ya baadhi ya mawifi, inafanya mawifi wote kuonekana wana tabia za ajabu. 

Mawifi wa namna hii mnatia aibu sana, kusemana wenyewe kwa wenyewe na hapo ndipo watu wengi
wanapokuwa wanajiuliza, ‘hivi kwa nini baadhi ya wanawake kwa wanawake huwekeana chuki bila sababu?’ Je, tangu kuumbwa kwa dunia ndivyo hali ilivyokuwa au ni wimbi tu la tabia ya baadhi ya wanawake kuoneana gere? Hii ni kwa sababu hata genge ambalo mhudumu wake ni mwanamke, kuna utafiti unaoonesha kuwa wateja wake wengi huwa ni wanaume. Ukiwauliza wanawake watakuambia anajiona, haongezi na maneno mengine yenye kumshusha mwanamke mwenzao. 


Hivi kama kaka yako amemchagua mwanamke huyo kuwa mkewe, wewe inakuhusu nini? Si usubiri na wewe uwe na mumeo uyaone? Kiukweli wenye tabia hizo jirekebisheni kwani mnakera na kushangaza mno! Mpenzi msomaji, napenda kukushukuru kwa kujitokeza kwenye Semina ya Mimi na Uhusiano iliyofanyika Jumamosi iliyopita. Usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook, Insta pia kujiunga na M&U kwenye Group la WhatsApp kwa namba hiyo hapo juu.

No comments