Header Ads

Zijue faida lukuki za zabibu

ASA ni msimu wa zabibu ambayo hujulikana kama chanzo kizuri cha divai, lakini pia huweza kuliwa kama tunda ambalo huwa katika kichana chenye zabibu sita  hadi 300. 


Matunda haya  yalianza kulimwa nchini Uturuki, lakini kwa hapa kwetu nchini yanapatikana sana mkoani Dodoma,  huwa na rangi nyekundu iliyoiva, nyeusi, bluu ya kukoza , njano, kijani na hata pinki.

 Zabibu ni moja ya tunda lenye sifa nyingi na nzuri zaidi kutokana na uwezo
wake wa kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hususan ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo. 


Pia zabibu husaidia damu kuwa nyepesi na kuifanya isigande ndani ya mishipa ya damu, hivyo mtumiaji wa zabibu hupunguza hatari ya kupata kiharusi (stroke). Tunda hili pia husifi ka kwa kutibu tatizo la upungufu wa damu, hususan kwa wanaotumia mara kwa mara tunda hili, huwasaidia kuepukana na ugonjwa wa bawasiri pia Zabibu ni tiba na kinga dhidi ya magonjwa ya ini kutokana na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi. Mbali na faida hizo, zabibu kutokana na kuwa na sukari yake ya asili, huweza kumsaidia
 

SUMU KATIKA DAMU.     
mtu katika kupunguza uchovu wa mwili na kutibu maumivu yasiyokuwa na sababu za moja kwa moja. Juisi ya zabibu ( au divai ) husaidia utumbo kufanya kazi kwa ufasaha zaidi na kuzuia ukavu wa haja kubwa , lakini pia divai huimarisha afya ya mishipa ya damu katika mfumo wa kumeng’enya, kusaga chakula na viini lishe.


 Lakini pia kutokana na madini yaliyomo ndani ya zabibu huifanya divai kuwa ni dawa nzuri inayopunguza maumivu ya tumbo yanayotokana na kujiminya kwa misuli ya kuta za matumbo (antispasmodic eff ect).

No comments