Header Ads

Aibu! Stand yaimaliza Yanga SC

HATIMAYE mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, wamesimamishwa. Yanga ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa jana dhidi ya Stand United, walijikuta wakifungwa mchezo wao wa kwanza baada ya Stand kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga 
 
Huu ni mchezo wa kwanza Yanga wanapoteza kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kucheza michezo mitano, ukiwa ni wa mwisho kabla ya kuvaana na watani wao wa jadi Simba, Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa. Haikuwa kazi ndogo kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo, kwa kuwa Yanga walipanga kikosi imara na kucheza kipindi cha kwanza vizuri, lakini makosa ya mabeki wake Vincent Bossou, na Haji Mwinyi, yalitosha kuwapa Stand bao safi katika dakika ya 58. 

Mshambuliaji wa Stand ambayo haijafungwa hata mchezo mmoja, Pastory Athanas, alitumia uzembe wa mabeki hao alipita katikati yao na kuifungia timu yake bao safi kwa shuti kali na kuifungia timu yake bao safi kwa shuti kali. Ushindi huu umewafanya Stand ambao wanafundishwa na kocha Mfaransa, Patrick Liewig, kukwea hadi nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, wakiwa na pointi 12 ambazo ni nne nyuma ya vinara Simba. Hata hivyo, Stand walionekana kuwa imara sana kwenye nafasi ya kiungo na ulinzi ambapo walitawala kwa sehemu kubwa sana huku wakicheza kwa nidhamu ya hali ya juu. Hii ina maana kuwa Yanga watakuwa wamepoteza mchezo mmoja mkoani, wametoka sare mmoja na kufungwa mmoja. Katika mchezo dhidi ya Ndanda

No comments