Header Ads

Amber Lulu adaiwa kutumika kwenye video chafu za X kufuatia picha zake kutumika kwenye CD

 
VIDEO Queen anayekuja kwa kasi Bongo, Lulu Augen ‘Amber Lulu’ anatuhumiwa kuhusika kwenye video chafu za X kufuatia picha zake kutumika kwenye CD mbalimbali zilizozagaa mtaani. Hilo lilibainika baada ya hivi karibuni mwandishi wetu akiwa kwenye mataa ya Ubungo jijini Dar kumshuhudia kijana mmoja anayeuza CD akionesha kwa siri sana moja iliyokuwa na kava lenye picha ya utupu ya mwanadada huyo huku akiinadi kwa siri akisema: “Za kikubwa blaza, buku tano tu!” 

Hata hivyo, baadaye iligundulika kuwa, CD hizo ni muendelezo wa matumizi ya picha za mastaa wa kike Bongo wenye tabia za kupiga picha chafu ambapo vijana hao huwatumia kwenye makava ya CD chafu licha ya ukweli kwamba ukienda kuangalia unakuta video ni wasichana wa nje ya nchi. 

Picha za mastaa ambazo kipindi cha nyuma zilikuwa zikitumiwa sana na vijana hao ni za Aunt Ezekiel, Wema Sepetu ‘Madam’, Husna Maulid, Gift Stanford ‘Gigy Money’ na wengineo. Alipotafutwa Amber Lulu na kuulizw     va kama anayo habari kuwa picha zake zinatumika kwenye CD chafu, mdada huyo ambaye hajambo kwa kupiga picha chafu alisema: “Mimi sijui bwana ila kama wanafanya hivyo ni wao na biashara zao.”

No comments