Header Ads

Amber Lulu: Young D kanipa gonjwa la moyo!

 
Video Queen maarufu Bongo, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ ameibuka na jipya akidai kuwa mwandani wake ambaye ni staa wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young D’ amempa gonjwa baya la moyo ambalo ameshauriwa na daktari wake kuwa asipokuwa makini anaweza kupoteza maisha. Akizungumza Amber Lulu alifunguka kuwa amekuwa akishindwa kujua endapo kutatokea kutoelewa kati yake na Young D nini kitatokea kwa sababu amekuwa akitumia muda mwingi kumfikiria, jambo ambalo limekuwa likimsababishia presha kushuka na sasa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo. 

“Nilikosana na D, nikawa sili chochote zaidi ya kunywa maji na kutumia muda mwingi kuwaza. Kuna siku nilianguka chumbani, nilipopelekwa hosptalini, daktari aligundua nina presha ya kushuka na vidonda vya tumbo lakini yote hayo ni kwa sababu ya Young D,” alisema Amber Lulu. Alisema daktari wake amemsihi kupunguza mawazo na pia ajitahidi kula kwa muda muafaka

No comments