Header Ads

Aunt Ezekiel, Wema, Irene Uwoya, Wolper VS Gigy Money, Lulu Diva, Amber Lulu nani zaidi!

KAMA wewe ni mfuatiliaji wa habari za mastaa utakubaliana na mimi kwamba, sasa hivi kumekuwa na ingizo jipya la warembo ambao wamekuwa hawakauki kwenye ‘media’ mbalimbali. Kama ni kuuza sura, wanauza kisawasawa na warembo hao wanaonekana kujipatia mashabiki kibao kutokana na staili yao ya maisha. Utakumbuka miaka ya nyuma akina Aunt Ezekiel, Wema Sepetu, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper na wengineo wakongwe walivyokuwa wanasumbua kwenye magazeti na hata mitandaoni. 
 
Walikuwa hawakaukiwi na skendo na wenyewe walikuwa wanachukulia poa, yaani skendo ilikuwa sehemu ya  maisha yao. Kupiga na kupigwa picha chafu kisha kusambaa wala halikuwa jambo la kushangaza sana lakini sasa hivi kama ‘wamesizi’ hivi. 
 
 ‘Viatu’ vyao sasa vimevaliwa na wadada kama vile Gift Stanford ‘Gigy Money’, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, Lulu Augen ‘Amber Lulu’,Pamella Daff a ‘Pam D’, Asha Salum ‘Kidoa’, Ericka Daniel ‘Erycah’, Tamari Ally ‘Tammy’, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ na wengineo. Hali hiyo inadhihirisha ule usemi usemao, kila kizazi na zama zake.
 
LULU DIVA
 Walikuwepo mastaa waliokuwa wasumbufu sana hapa Bongo kama vile Christina Manongi a.k.a Sinta au J-Lo wa Bongo, Nuru Nasoro ‘Nora’, Ruth Suka ‘Mainda’, Blandina Chagula ‘Johari’, Salama Salmin ‘Sandra’, Happiness Wenslaus ‘Nyamayao’ na wengineo wa kizazi hicho unaowakumbuka.

 Lakini sasa hivi hawapo kwenye ulimwengu wa mastaa wasiokauka kwenye media. Sisemi wamechuja au wamepitwa na wakati, no! Ni kwamba zama zao zimepita, zikaja zama za akina Wema wanaohiti mpaka sasa na pia wameibuka hawa akina Gigy Money.

No comments