• Latest News

  September 26, 2016

  Azam: Ndanda walipata bahati tu

  MARA baada ya Azam kupokea kichapo cha pili katika ligi mbele ya Ndanda ya Mtwara, uongozi wa timu hiyo umeibuka na kudai kwamba hakuna wa kumlaumu kutokana na
  kichapo hicho kwa sababu wapinzani wao waliwazidi bahati tu ambayo ndiyo iliwasaidia kupata ushindi huo.
   
  Azam chini ya kocha wake, Mhispania, Zeben Hernandez, juzi Jumamosi ilijikuta ikiendeleza rekodi yake ya kupoteza katika Uwanja wa Nang’wanda Sijaona, Mtwara
  mara baada ya kuchapwa mabao 2-1 mbele ya wenyeji wao Ndanda ya mkoani humo.

  Akizungumza na Championi Jumatatu, Msemaji wa Azam, Jaffar Idd, alisema kwamba licha ya wao kupambana kwa ajili ya kusaka ushindi kwenye pambano hilo, bahati haikuwa ya kwao kutokana
  na nafasi nyingi za mabao walizozitengeneza kuishia mikono mwa kipa wa Ndanda na nyingine kuokolewa na mabeki.

   “Kiukweli hatuna wa kumlaumu kutokana na kipigo hiki cha Ndanda kwa sababu sisi tulikuwa bora zaidi ya wapinzani wetu ambao muda mwingi tulikuwa tunawashambulia lakini ndiyo hivyo, mwisho wao wameibuka vinara kwa kutufunga kibahati kwa sababu tuliwazidi kwa kila
  kitu. “Bado hatuna wasiwasi wowote juu ya kufanya vizuri licha ya kwamba tumepoteza mechi mbili mpaka sasa kwa sababu kuna mechi nyingi zimebaki na kocha Zeben ameshayachukua mambo yote ambayo yamesababisha sisi kupoteza mechi hizi na ametuhakikishia kwamba tutaibuka washindi katika mchezo ujao,” alisema Idd
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Azam: Ndanda walipata bahati tu Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top