• Latest News

  September 03, 2016

  BAADA NGASSA KUVUNJA MKATABA SAUZ, HII NDIYO KAULI YA KOCHA WA YANGA...

  NGASSA

  Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amempa ugumu aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Free States ya Afrika Kusini, Mrisho Ngassa kurejea kuichezea timu hiyo.

  Hiyo, ni siku moja tangu taarifa za kiungo huyo kusitisha mkataba wake wa kuichezea Free States kwa makubaliano huku tetesi zikienea kuwa nyota huyo atarejea kucheza Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo la Ligi Kuu Bara msimu huu.

  Ngassa, alisitisha mkataba wa kuendelea kukipiga Sauz kwa kile alichodai kuwa timu hiyo haina malengo ya kutwaa ubingwa zaidi kushiriki kwenye ligi kuu.

  PLUIJM
  Pluijm alisema kwenye kikosi chake hahitaji kiungo mshambuliaji kwani tayari anao wanne, tena vijana wenye uwezo mkubwa wa kuendana na kasi yake.

  Pluijm aliwataja viungo hao washambuliaji kuwa ni Mzambia, Obrey Chirwa, Juma Mahadhi, Simon Msuva na Deus Kaseke ambao anaamini bado wana uwezo mkubwa wa kuichezea timu hiyo kwa muda mrefu kutokana na umri wao.

  Aliongeza kuwa, haoni sababu ya kujaza viungo wengi washambuliaji kwenye kikosi chake kutokana na kutokuwa na tatizo katika nafasi hiyo.

  “Nimepata taarifa za Ngassa kusitisha mkataba wake wa kuichezea Free States, labda nikwambie tu, ni ngumu kwangu kusajili kiungo mshambuliaji katika kikosi changu kwa hivi sasa, kwani tayari ninao wanne ambao ni vijana wenye uwezo mkubwa wa kucheza.


  “Wachezaji wanaocheza nafasi hiyo (ya Ngassa) ni Chirwa, Mahadhi, Kaseke na Msuva, wote ni wazuri. Tofauti na kasi yao ya kushambulia, pia wana uwezo wa kufunga mabao, ni aina ya uchezaji aliyonayo Ngassa,” alisema Pluijm.

  SOURCE: CHAMPIONI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: BAADA NGASSA KUVUNJA MKATABA SAUZ, HII NDIYO KAULI YA KOCHA WA YANGA... Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top