• Latest News

  September 30, 2016

  CHANZO CHA NDEGE YA RONALDO KUPATA AJALI JIJINI BARCELONA CHABAINISHWA


  Ndege ya mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo imepata ajali mjini Barcelona, Hispania.

  Ndege hiyo imepata ajali kwa kuteleza hadi kukwama kwenye majani na imeelezwa sababu ya ajali hiyo ni kuvunjika kwa gia ambayo hutumika wakati wa kutoa.

  Ronaldo hakuwa katika ndege hiyo wakati ikitua Barcelona na kupata ajali hiyo, ila imeelezwa, tatizo hilo la gia ndiyo limekuwa chanzo.


  Hakukuwa na taarifa za majeruhi na ndege hiyo haikuumia zaidi ya kukwama kwenye majani ingawa imeelezwa matengenezo yake, bado yatakuwa na gharama za juu.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: CHANZO CHA NDEGE YA RONALDO KUPATA AJALI JIJINI BARCELONA CHABAINISHWA Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top