Header Ads

Cherekochereko na vilio humohumo!...SIKU YA NDOA YAO SHAMSA, MUMEWE VILIO KISA KIPO HAPA

Cherekochereko na vilio humohumo! Ijumaa iliyopita ilikuwa ni siku ya furaha kwa staa wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford na mumewe ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa nguo jijini Dar, Rashid Said ‘Chid Mapenzi’ kufuatia kufunga ndoa, lakini cha ajabu waliwaachia maswali waalikwa kutokana na maharusi hao kuangua vilio muda mwingi, Wikienda lina hatua kwa hatua.

 KWANZA NDOA Ndoa ya wawili hao ilifungwa katika Msikiti wa Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar na kufuatiwa na sherehe (harusi) iliyofanyika siku hiyohiyo nyumbani kwa wazazi wa Shamsa, Sinza-Afrika Sana na baadaye wageni waalikwa wakaelekea Upanga kwa upande wa mwanaume. 

SHEREHE YAANZA Sherehe hiyo ilianza kwa shamrashamra ambapo baadhi ya wasanii na watu mbalimbali walihudhuria huku wakiburudishwa na mawaidha ya dini sanjari na muziki wa kaswida uliokuwa ukipigwa nyumbani kwa wazazi wa Shamsa.

 SHAMSA AANZA Awali, baada ya kuingia kwenye chumba cha harusi akitokea saluni, Shamsa alianza kuangua kilio hata kabla bwana harusi hajafika kwa ajili kufunga ndoa ambapo alikataa mtu kuingia chumbani humo kwa madai kwamba, anahitaji kupumzika lakini huku akiendelea kulia. “Shamsa analia sana sijui kwa nini? Na amesema hataki mtu kule chumbani kwa sababu anahitaji kupumzika mpaka watakapokuja hao wa upande wa bwana harusi na mashehe kwa ajili ya kuwafungisha ndoa,” alisema mmoja wa wanafamilia. 

BWANA HARUSI NAYE Baada ya muda, bwana harusi aliingia nyumbani hapo akiwa na wapambe wake na mashehe ambapo waliingia kwenye chumba alichokuwa Shamsa kwa ajili ya kufunga ndoa ambako huko nako patashika iliibuka, kwani bwana 
harusi huyo naye alianza kulia kilio cha kama mtoto mdogo!

 MAHARUSI NJE, VILIO TENA Baada ya zoezi la kufunga ndoa (na kulia) kumalizika maharusi hao walishuka chini kutoka ghorofani ambapo tukio la utambulisho lilianza.  Shamsa ndiye aliyekuwa wa kwanza kutambulisha nduguze lakini huku akianza tena kulia, wakati mwingine sauti yake ilishindwa kutoka vizuri kutokana na ile kwikwi ya kilio. Bwana harusi kuona hivyo, naye akaanza kuyamwaga machozi kama wanaoshindana vile! 

BWANA HARUSI ETI ANA AIBU! Ilipofika zamu ya bwana harusi kuwatambulisha ndugu na jamaa zake, alishindwa kwa kile kilichosemwa na watu chini kwa chini kuwa, eti ana aibu sana (sijui alimtokeaje Shamsa). Ikabidi kazi hiyo aifanye baba yake. 

HARUSI YAHAMIA UPANGA, MAMBO YALEYALE! Baadaye sherehe za harusi zilitoka Sinza Afrika Sana na kuhamia Upanga nyumbani kwa baba wa bwana harusi ambako kulikuwa na kuserebuka kwa sana. Lakini cha ajabu, paparazi mmoja alipomfuata bwana harusi huyo na kumuuliza jina lake kamili, alijibu huku akilia: “Niache bwana, mi nimechanganyikiwa huko.”

MASWALI YA WAALIKWA Baadhi ya waalikwa walichukua muda mrefu kuulizana kisa hasa cha wanandoa hao kutumia muda mwingi kulia badala ya kuonesha tabasamu. “Jamani! Hawa maharusi mbona wanalialia sana. Kitu kidogo machozi. Huyu anaulizwa jina lake lote, analia, anasema aachwe amechanganyikiwa. Amechanganyikiwa na nini sasa?” 

SHAMSA ATAFUTWA AKIWA FUNGATE Kutokana na kuwa bize na shughuli, Wikienda lilishindwa kumtafuta bibi harusi huyo kwa siku hiyo, lakini Jumamosi, akiwa fungate katika eneo ambalo halikutajwa, alipigiwa simu ili kupata maneno yake ya ni kipi hasa kilikuwa kikimliza siku ya ndoa, lakini simu yake iliita bila kupokelewa. 


VIJEMBE VYATAWALA Kwenye shughuli hiyo mshehereshaji ‘MC’ alikuwa msanii wa sinema, Jimmy Mafufu aliyekuwa akitoa vijembe vikali kwa wasanii wa kike, akiwataka waige mfano wa mwenzao na si kuendelea kuvunja amri ya sita ya Mungu. “Jamani niwaambie tu wasanii wa kike kwamba mnatakiwa kuolewa, tambueni kuwa wakati utafika na hizo make up zenu zitadunda. Yaani miaka i n a e n d a , a c h e n i kujiachia tu na vijana bila ndoa. Shamsa ameleta heshima k w a t a s n i a kutokana na uamuzi w a k e , ” a l i s e m a Mafufu. 

HAINAGA USHEMEJI YATAWALA Katika sherehe hiyo wimbo wa msanii wa Singeli, Man Fongo, Hainaga Ushemeji Tunakulaga ulitawala kwani kila wakati wageni waalikwa walikuwa wakiuomba wapigiwe wimbo huo kwa staili ya ‘once more’ huku vijembe vikiendelea bila kutaja mlengwa. 

No comments