Header Ads

Diamond ‘amdis’ Kiba akinunua nyumba 3

 
HABARI ya mjini ambayo huenda huifahamu ni kwamba, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amenunua nyumba tatu kwa mpigo maeneo ya Tabata Segerea, jijini Dar kisha baadaye kikasambaa ‘kiklipu’ ambacho ‘dizaini’ kinaonesha jamaa huyo ‘akimdis’ kimtindo mpinzani wake, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.
 
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika ambacho kilikuwepo kwenye ununuzi huo, Diamond alifanya jambo hilo la kupongezwa mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo alikuwa ameongozana na mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Dalali Mwanamke na dansa wake, Moze Iyobo. “Kusema ukweli jamaa anajua kuwekeza kwenye nyumba, juzi kafanya kufuru nyingine kwa kununua nyumba tatu kwa mpigo zenye thamani ya shilingi milioni 300,” kilidai chanzo hicho.

‘Amdis’ kimtindo Ali Kiba Baada ya tukio hilo kufanyika, mtandaoni ilisambaa ‘klipu’ inayoonesha Diamond akiwa kwenye nyumba hizo kisha inasikika sauti yake akiimba wimbo unaodaiwa ni dongo kwa Kiba. Sehemu ya maneno hayo inasema; “Sasa waambie dada zao wa Kariakoo nao waje Ulaya.” Kwa nini inadaiwa wimbo huo ni dongo kwa Kiba? Inadaiwa kuwa, wimbo huo ni
dongo kwa King Kiba ambaye anamkimbiza kimafanikio kwa kuwa, Kiba anatokea Kariakoo hivyo Diamond anamtaka naye awapeleke dada zake Ulaya. Alipotafutwa Kiba ili kumsikia anazungumziaje madongo hayo, simu yake iliita bila kupokelewa. Diamond amekuwa akinunua nyumba kila wakati ambapo licha ya kuwa na ile aliyoijenga kule Madale jijini Dar, anazo nyingine maeneo ya Mbezi ya Kimara, Mwananyamala na sehemu nyingine

No comments