Header Ads

Dola za Jack Pemba zampa wehu Vai!

BAADA ya Global Publishers kuchapisha habari za Isabela Mpanda kula maisha na Jack Pemba nchini Uganda hivi karibu, inadaiwa kuwa msanii wa fi lamu za Kibongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ amepagawa, kiasi cha kuanza kuhaha kupata mawasiliano na mpenzi huyo wa zamani wa Aunt Ezekiel.
 
 Kilichompagawisha Vai ni lile burungutu la dola zilizoonekana zimeshikwa na Jack Pemba, wakati alipopiga picha na msanii huyo wa fi lamu na muziki, aliyekwenda
nchini humo kwa mwaliko wake, akiwa na kundi lake la Scorpion, linalowajumuisha pia Baby Madaha na Jini Kabula. 


“Dah nyie kiboko, mmejuaje habari hizo? Ukweli ninamtafuta sana Jack Pemba maana yale madola siyo ya mchezo, nayatamani kweli,” alisema Vai baada ya Za Motomoto News, kumtafuta na kutaka kupata ukweli wa ubuyu uliozagaa mtaani.

No comments