Header Ads

Ester Kiama Atajwa Kujiuza, ang’aka


ester-kiama-4
Muigizaji mrembo anayepanda kwa kasi kwenye gemu la filamu Bongo, Ester Kiama akifanya mahojiano na Boniface Ngumije (kushoto).
BAADA ya wiki iliyopita katika safu hii kukuletea muuza sura kwenye video za Kibongo, Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ leo hii Mtu Kati imepiga misele mpaka Mitaa ya Kijitonyama jijini Dar yanapopatikana makazi ya muigizaji mrembo anayepanda kwa kasi kwenye gemu la filamu Bongo, Ester Kiama.
Mwanadada huyu ambaye kwa mara ya kwanza alianza kufahamika kupitia filamu ya Anko Kiepe kwenye makala haya anafunguka mambo mengi kuhusu kazi zake pamoja na maisha yake halisi.

Mtu Kati: Kwa kuanza ni vyema ukawaeleza wasomaji wetu mpaka sasa umefanya muvi ngapi zako mwenyewe na zile ulizoshirikishwa?
Ester Kiama: Nimeonekana kwenye filamu nyingi, baadhi yake ni Anko Kiepe, Mhanga, Profesa na nimeshirikishwa nyingi tu.
ester-kiama-1
Ester Kiama akiwa katika pozi baada ya mahojiano.
BONGO MUVI IMEDORORA?
Mtu Kati: Unafikiri tatizo ni nini mpaka soko la filamu linadorora?
Ester Kiama: Waigizaji wengi hawajitumi. Namaanisha ni wachache sana wanaoweza kutafuta uhalisia wa muvi zao kwa kuanzia muonekano wao au kuyatafuta mazingira ambayo muvi zao zinafaa kurekodiwa.
Kwa mfano; kwenye uhalisia unakuta mwanadada staa kabisa anatakiwa kucheza akiwa kwenye mazingira ya kijijini tena kutoka familia ya kimaskini, lakini anacheza kwa sababu muvi inamtaka kufanya hivyo, jambo la kushangaza unakuta amechora tatoo. Unaweza kuona wanavyoukimbia uhalisia, hivyohivyo katika mambo mengine mengi hukosea sana ndiyo maana filamu zetu zinashuka thamani kila kukicha.
Mtu Kati: Kwa upande wako changamoto ipi kubwa unaipata unapokuwa unaandaa muvi?
Ester Kiama: Nafikiri ni soko la kuuzia baada ya kuandaa filamu yangu. Unajua wakati mwingine mtu unamtaji mkubwa ambao ukiupigia hesabu unaona kabisa unaweza kufanya kitu kikubwa. Lakini kwa kuwa soko letu la filamu ni dogo inakuwa changamoto kufanya hivyo, so mara nyingi huwa nalazimika kufanya chini ya kiwango kutokana na soko linavyo-nitaka. Siwezi kutoa milioni hamsini kuandaa filamu Bongo na ikarudi yote nipate na faida, hilo jambo si rahisi.
ester-kiama-3
…Mapozi yakiendelea.
Mtu Kati: Bajeti yako pindi unaandaa filamu huwa ni shilingi ngapi?
Ester Kiama: Inategemeana na stori ya muvi, wakati mwingine huwa naandaa filamu mpaka milioni 20.
dude2.gif
Msanii mkongwe wa filamu Kulwa Kikumba ‘Dude’ alipokuwa akifanya mahojiano na Global TV.
ALIO-TOKA NAO KIMA-PENZI VEE-PE?
Mtu Kati: Ume-wahi kutoka kima-penzi na wasanii wenzako au mastaa wangapi?
Ester Kiama: Hahaaa! (anacheka huku akiinamisha kichwa chini) Umeanza mambo yako, sijawahi hata mara moja, sipendelei sana kutoka na hao watu!
DUDE JE?
Mtu Kati: Lakini inasemekana unapika na kupakua na msanii mwenzako Kulwa Kikumba ‘Dude’ kiasi kwamba ametelekeza familia yake kisa wewe!
Ester Kiama: Hakuna ukweli wowote juu ya suala hilo. Mimi na Dude tupo karibu kwa sababu ya kazi, lakini kuhusu familia yake, ninachojua ameoa na mambo mengine aulizwe mwenyewe!
Mtu Kati: Kuna tetesi kuwa masuala hayo ya kikazi yanawafanya mpaka mnapiga kambi kwa siku kadhaa nyumbani kwako mkijiachia kwa raha zenu tena wakati mwingine mkiwa wawili tu!
ester-kiama-2
Ester Kiama akiwaza jambo.
Ester Kiama: Mwandishi, elewa kwamba Dude ni mtu ambaye ninafanya naye kazi. Kuja nyumbani kwangu si ajabu na ikitokea hivyo ni kwa ajili ya masuala ya kikazi tu hakuna kingine!
Mtu Kati: Je, Dude amewahi kukutaka kimapenzi?
Ester Kiama: Jamani kwani hakuna maswali mengine! Nimeshakwambia Dude ni mshikaji wangu atanitakaje kimapenzi na wakati yeye ana familia yake?
ANAYEVUTIWA NAYE
Mtu Kati: Staa gani anakuvutia kutoka naye kimapenzi?
Ester Kiama: Sijawahi kufikiria juu ya hilo so jibu lake linakuwa gumu kulitoa.
SKENDO YA KUJIUZA JE?
Mtu Kati: Inasemekana una skendo ya kujiuza na kujirahisisha kwa mapedeshee?
Ester Kiama: Ni maneno tu ya watu. Nawezaje kujiuza wakati kama ni pesa nina biashara zangu ambazo zinaniingizia kipato na kunifanya niishi nitakavyo. Kuhusu kujirahisisha kwa mapedeshee siwezi kuwa ‘cheap’ kiasi hicho. Mimi ninajielewa na labda hao mapedeshee ndiyo wanasumbuka na mimi, kifupi sina hata mpango nao.
RAY2334
Msanii mkongwe wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’.
WA KUFANYA NAYE KAZI JE?
 Mtu Kati: Staa gani ambaye unatamani kufanya naye kazi?
Ester Kiama: Ray ananivutia sana.
Mtu Kati: Oke Ester nashukuru kwa kukubalia kuhojiana nami, nakutakia kazi njema.
Ester Kiama: Nashukuru pia.

No comments