Header Ads

FIESTA MORO YAMVISHA SUTI STAMINA, PICHA SI ZA KUKOSA ZIPO HAPA ZOTE

Stori: Mwandishi Wetu Morogoro
SHOO ya Fiesta 2016,juzikati ilimvisha suti msanii wa muziki wa kufoka foka kutoka mkoani hapo Stamina, kiasi cha kuwafanya baadhi ya wasanii wenzake kumtania kwa kumwambia kuwa atakua amepania kuwakomoa.

Tukio hilo lilitokea ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini hapo ambapo Msanii huyo alipanda jukwaani hapo akiwa ni msanii wa pili baada ya ratiba ya wasanii wakubwa kuanza ambapo alitanguliwa na Chrisian Bella.
Stamina alifanya makamuzi ya nguvu na kujikuta muda wote akipata shangwe nyingi kutoka kwa ndungu zake hao huku akifuatiwa na Vanessa Mdee ambaye naye alifanya makamuzi yake huku akifuatiwa Mr Blue ambaye alikuwa akifanya makamuzi yake ya kufunga shoo takribani siku zote tangu tamasha hilo lilipoanza kurindi kwa mara ya kwanza jijini Mwanza ambapo lilizinduliwa.
Ratiba ya shoo iliendelea kuteka hisia za mashabiki kwani baada ya Mr Blue alipanda mtoto wa mama Saidi Chege aliyefanya makamuzi ya nguvu huku akimpisha Sholo Mwamba, ambaye alitumia jukwaa hilo kuutambulisha muziki wa Singeli kisha kumuachia jukwaa mkongwe wa burudani Mr Msifa Dully Skes ambaye naye aligonga ngoma zake kisha kumuachia uwanja huo mtoto wa Morogoro Belle9.
Makamuzi hayakuishia hapo kwani ukiangalia ratiba na wingi wa wasanii wote waliopanda ungeweza kusema hata nusu ya waliyokuwa bado hawakuifikia kwani baada ya Belle 9 ndiyo kwanza ratiba mpya ilifunguliwa na Hamadai kwa kuruhusu muziki wa Bendi ambapo alipanda na wimbo wa Ipo siku yangu tu wa God luck Gobert.
Bendi ilizidi kupamba moto kwani Hamadai aliimba sambamba na Nandy huku Maua Sama akisimama kidete kuitikia baadhi ya kolasi za wimbo nyimbo hizo hadi pale ngoma ilipo pamba moto na watatu hao kuamua kushuka na kumuachia jukwaa alitawale, Baraka Da Prince.
Usiku huo ulikuwa wa aina yake hasa ukilinganisha na wasanii walivykuwa wakipishana ambapo baada ya Baraka Da Prince kutoka alichukua kipaza sauti hicho Ben Pol, ambaye naye alifanya vilivyo hadi pale Jux alipopanda na kuimba wimbo wao wa Nakuchana wa pamoja kisha kushuka wote na kumuachia jukwaa Darasa.
Hapo ndiyo muziki wa kufoka foka ulipochukua nafasi kwa mara nyingine tena kwana baada ya Darasa alipanda mwamba wa kanda ya ziwa Faridi Kubanda ‘Fid-Q, kisha kukitimua vilivyo hadi pale naye alipoamua kumuachia jukwaa hilo Manfongo.
Singeli nayo iliwanogesha mashabiki wa burudani kwa kiasi kwani baada ya Manfongo alipanda Snura ambaye naye alitumia jukwaa hilo kutikisa chura wake kiasi cha kuwapagawisha mashabiki wa Morogoro na kuwaachia kijiti cha burudani hizo crow ya Weusi ambao kwa pamoja walifunga burudani za Fiesta mjini hapo.
Wikiendi hii Fiesta inatarajiwa kuendelea katika mikoa ya Tanga na Moshi ambapo ratiba inasema kwamba siku ya Ijumaa ya Septemba 23 makamuzi ya Fiesta yataendelea ndani ya Uwanja wa Mkwakwani Tanga kisha jumapili ya Septemba 25 katika uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Wasanii watakao tumbuiza kwenye shoo hizo ni pamoja na Weusi,Shetta,Mr Blue,Manfongo,Ben Pol,Christian Bella,Maua Sama,Nay wa Mitego,Snura,Madee, Navykenzo, Darasa,Dogo Janja,Jambo Squad, Barnaba, Makomando,Nedy Music, Sholo Mwamba na Hamadai.


No comments