Header Ads

FURSA YAONGEZA THAMANI MARADUFU SINGIDA


DARASA la Fursa mapema leo limeendelea ndani ya Ukumbi wa Kisamaka uliyopo ndani ya Hoteli ya Aqua Vitae mjini Singida, ambapo watoa maaada mbalimbali akiwepo Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba, Mrisho Mpoto, Nikki wa Pili, Mkurugenzi wa Chuo cha Mlimani Profession Hassani Ngoma na Meneja wa Bidhaa wa NMB wa Singida Shamim Ally.
Wakizungumza na kutoa mbinu mbalimbali za mafanikio kwenye darasa la Fursa mapema hii waongeaji hao, waliwapatia mbinu mbadala wakazi hao huku wakiwataka wasikilize sauti zao na miyo yao kwa kila uamuzi wanaoupanga.
1
Baadhi ya watoa maada wa Fursa wakiwa kwenye picha ya pamoja mbele ya meza wakati semina hiyo ikiendelea ndani ya Ukumbi wa Kisamaka katika Hoteli ya Aqua Vitae mjini Singida mapema leo.
2
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba akiwapa mbinu za kuongeza thamani wakazi waSingida kwa kutumia semina ya Fursa.
3
Msanii wa Bongo Fleva Nikki wa Pili akitoa neon kwenye semina ya Fursa.
4
Mshereheshaji wa semina ya Fursa Mwijaku akijaribu kuwafafanulia neno baadhi ya wadau waliyojitokeza kwenye semina hiyo.
5
Mkurugenzi wa chuo cha Mlimani Profession Hassani Ngoma akiwaonyesha Fursa wakazi wa Singida waliojitokeza.
6
Meneja wa Bidhaa wa NMB mkoa wa Singida Shamim Ally akiwapa mbinu za kujiunga na benki hiyo ili waweze kupata mikopo ya kuwaendeleza kwenye shughuli zao za kilimo.
7
Meneja Masoko wa Bima Mkoa wa Singida Yasini Kaali akiwahusia wakazi wa Singida namna ya kujiunga na bima mbalimbali ambazo zinaweza kuwasaidia kwenye shughuli zao za kiuchumi.
8
Msanii wa mashairi ya kughani, Mrisho Mpoto akijaribu kuwafungulia fursa wakazi wa Singida kwa kuwapatia mifano mbalimbali.
9
Sehemu ya umati uliyojitokeza kusikiliza na kujifunza mambo mbalimbali yatokanayo na wazungumzaji wa semia ya Fursa mapema leo mjini Singida.

No comments