Header Ads

Hainaga Ushemeji Afande Laivu na Mke Wa Mdogo Wake Gesti

DAR ES SALAAM: Wimbo wa msanii wa Singeli, Man Fongo wa Hainaga Ushemeji ndiyo habari ya mjini kwa sasa ambapo mashairi yake hivi karibuni yalitimia kufuatia askari wa Gereza la Ukonga jijini hapa, Kassim Juma kudaiwa kunaswa chumbani gesti akiwa na mke wa mdogo wake aliyejitambulisha kwa jina la Haroub, aitwaye Rukia Clemens, Amani lilidokezwa na kuibukia kwenye tukio. Ishu hiyo yenye viashiria vya kusambaratisha ukoo, ilijiri Septemba 26, mwaka huu kwa maana ya Jumatatu iliyopita, kwenye chumba namba nne cha gesti iliyopo Ukonga ya Majumba 6, Dar. Afande Kassim alikumbwa na kasheshe hilo akiwa tayari chumbani na shemejiye huyo bila kujua kuwa, alikuwa ndani ya bomba ambalo limezibwa kotekote hivyo haikuwa rahisi kutoka.

AMANI LILIPATAJE ISHU?
 Ni wakati gazeti hili likikatiza kuelekea kwenye mihangaiko ya kila siku, ndipo lilipomwona Haroub akiwa ameongozana na askari wawili wa usalama barabarani na kutonywa kuwa, wa
nakwenda kumnasa afande huyo akiwa na shemeji yake. Gazeti hili liliunga msafara huo mpaka kwenye gesti hiyo ili kushuhudia fumanizi hilo likiwa limesimamiwa na maafande hao, huku mume wa Rukia akiwa katika hali ya jazba kali.

AFANDE ALIVYONASWA
Baada ya kufika, mtu mmoja aligonga mlango wa chumba namba nne ambapo mlalamikiwa huyo alipouliza ni nani, alijibiwa kuwa ni mhudumu amepeleka sabuni ya kuogea. Mlalamikiwa huyo alifungua mlango kidogo na kutoa mkono ili kuipokea sabuni hiyo na ndipo waliokuwa nje waliposukuma mlango na kuzama ndani ya
chumba, sambamba na mpigapicha wetu.

AFANDE APIGWA MASWALI
Baada ya kuwa chini ya ulinzi, afande huyo aliulizwa maswali kadhaa kama ifuatavyo: Trafiki: “Habari yako?” Afande Kassim: “Salama afande.” Trafiki: “Unaitwa nani?” Afande Kassim: “Naitwa Kassim Juma.” Trafiki: “Huyo uliyenaye ni nani yako?” Afande Kassim: “Shemeji yangu.” Trafiki: “Na huyu hapa unamjua?” Afande Kassim: “Ndiyo namjua, huyo ni mdogo wangu ambaye huyu ni mkewe.”

 Trafiki: “Sasa mnataka kufanya nini hapa kitandani?” Afande Kassim: “Jamani naomba mnisamehe, siyo amri yangu ni ibilisi tu alinipitia halafu mimi ni poti mwenzenu.” Mlalamikiwa huyo alijitambulisha kuwa, yupo Magereza Ukonga na kusema ana kitambulisho. Katika mbilinge hilo, mume wa Rukia alitaka kwenda mbele zaidi na kumuangushia kipigo kaka yake lakini alidhibitiwa na trafiki hao.

ALICHOAMUA MDOGO MTU Baada ya zoezi hilo kukamilika, Haroub alisema hana sababu ya kumpeleka kaka yake polisi ila anachoomba apewe mkewe arudi naye nyumbani
kwa vile alishamjua mbaya wake ni nani!

HUU NDIYO UDUGU WAO Akizungumza na gazeti hili kuelekeza mazingira ya fumanizi hilo la kaka yake, Haroub alisema: ”Huyu Kassim ni kaka yangu kabisa, mtoto wa mama yangu mdogo. Alitoka kijijini kule Mafia baada ya kumaliza kidato cha nne na kuja hapa Dar ambapo alifikia nyumbani kwetu, Tandika. “Mama yangu mzazi ambaye ni mama yake mkubwa ndiye aliyemfanyia mpango wa kujiunga na mafunzo ya JKT (Jeshi la Kujenga Taifa). Na mimi ndiye niliyempeleka mpaka kwenye vipimo pale Ruvu JKT. “Baada ya kumaliza mafunzo ya JKT  alipata nafasi ya ajira katika Jeshi la Magereza anapofanya sasa hapo Ukonga ambapo anaishi na mkewe. “Kinachoniuma zaidi mimi ndiye niliyemuonesha maeneo mbalimbali hapa Dar, ikiwemo Uwanja wa Taifa, Posta, Feri, Ikulu na maeneo mengine.
Nakumbuka alinishukuru sana. Lakini leo hii ananigeuka? Yaani siamini.”

KUMBE ULIKUWA MTEGO “Iko hivi, siku moja mke wangu Rukia aliniambia kuwa shemeji yake anamtumia meseji ambazo zinavuka mipaka ya ushemeji. “Ingawa mke wangu alimtilia shaka lakini aliendelea kuchati na shemeji yake akimrudishia majibu yaliyopoa lakini kaka alizidi kumtumia vijimeseji vyake. “Siku moja, kaka alimpasulia wazi, mke wangu hakuamini alichoambiwa hivyo alinieleza mimi mumewe na kunionesha meseji zote. Ili kunithibitishia, mke wangu alimpigia simu bro ili nisikie sauti yake. Kweli nilimsikia vizuri sana. Na ndipo tukaandaa mtego wa kumnasa gesti.”

KWA NINI TRAFIKI? Haroub alisema kuwa, baada ya kaka yake na shemejiye kuingia kwenye
gesti hiyo, aliamua kuwafuata trafiki hao waliokuwa eneo la kuongozea magari eneo la Ukonga na kuwaomba kwenda kumsaidia. “Walisema wao hawahusiki na mambo ya fumanizi, lakini nikawaambia kwamba kama hawataki, mimi nakwenda kumfumania mwenyewe, kitakachotokea, kama ni kuua, kumwaga damu au kufanyaje, wao watawajibika kwa sababu nimewaambia wakakataa kunipa msaada, ndipo wakakubali kuongozana na mimi.”

FAMILIA YAPIGWA BUTWAA, HAIAMINI “Kusema ukweli, kila ndugu niliyemwambia hajaamini. Mama haamini pia, kila mtu amepigwa na butwaa. Wanauliza kweli Kassim anaweza kufanya hivi kwa shemeji yake? Awali walijua mke wangu anamsingizia,” alisema Haroub akiwa anaondoka na mkewe kuelekea nyumbani kwake huku akilia na mkewe akimbembeleza.

No comments