Header Ads

Hongera Shamsa, ila ustaa uishie mlangoni

‘ACTION…camera roll’ ndiyo maneno ambayo wasanii huyatumia mara kwa mara wanapokuwa lokesheni, eneo ambalo wanalitumia kurekodi kipande fulani cha sinema zao.
 
Huwa wanayatamka maneno hayo ili waweze kuuvaa uhusika wa kifi lamu. Yaani kama anatakiwa kuonekana analia, msanii ajitoe ufahamu kwa muda ili aonekane analia mbele ya kamera. Mathalani, anaweza kuvaa uhusika wa tabia za mlinzi wakati yeye si mlinzi.

 Kwa tafsiri rahisi ni kwamba anachokifanya pindi anapoambiwa maneno hayo huwa si uhalisia. Anakuwa anaigiza. Anavaa uhusika wa jambo fulani baadaye anarudi kwenye hali yake ya kawaida. Huo ndiyo msingi wa mimi leo kumuandikia barua nzito muigizaji mwenye umbo la kuvutia, aliyejaajaa mwili, mwenye rangi ya ‘chokoleti’, mtoto wa mzee Ford, wa kuitwa Shamsa.

 Awali, nianze kwa kukupongeza. Umefanya uamuzi wa busara sana kuingia kwenye chama cha wenye ndoa, umemkabidhi moyo wako kijana mtanashati na mchakarikaji wa mjini, Chid Mapenzi. Najua hadi kufi kia hatua hiyo, unayo mapito mengi, lakini mwisho wa siku, nyinyi sasa ni mke na mume.
Kama nitakuwa sahihi, hamkuchukua muda mrefu sana kwenye uchumba. 


Sina hakika kama mmefi kisha hata miezi sita lakini hilo haliondoi dhana nzima ya muunganiko wenu. Mlikaa, mkatafari na mwisho mkaona hakuna sababu ya kuendelea kuwafaidisha wamiliki wa nyumba za wageni. Mkachagua kuishi pamoja, mpike na kupakua bila kuulizwa na mtu. Hongereni sana! Baada ya pongezi hizo, acha nihamie upande wa pili wa barua yangu; ‘ndoa na ustaa’. 

Nimeona nikutahadharishe mapema. Ni vitu viwili tofauti. Chondechonde usithubutu kuchanganya vitu hivi. Ni hatari. Dada yangu, unapokuwa nyumbani kwa mumeo yale mambo ya utani wa lokesheni achana nayo kabisa. Zile  za kuitana ‘baby’ mnapokuwa lokesheni, hupaswi kuzifanya
unapokuwa na mumeo nyumbani. 


Achana na mambo ya kufuga kucha ndefu halafu eti ukawa mtu wa kupikiwa kila siku na hausigeli. Ikiwezekana chakula cha mumeo mpikie mwenyewe. Kupikiwa na mkeo nako kuna raha yake. Kunaongeza upendo pia, hata kama unatingwa na kazi zako lakini tenga siku za wewe kuingia mwenyewe jikoni na kumkorofi shia shemeji yetu. Usitumie mwanya wa kazi zako kufanya mambo ambayo hayatamfurahisha mwenzio.

 Jiheshimu. Uigizaji uwe na mipaka. Siyo unaruhusu waigizaji wenzako wakutanie kiasi cha kuondoa thamani ya kuwa mke wa mtu. Weka mipaka ya kazi na ndoa. Mashosti
zako wasiwe madereva wa ndoa yenu. Wasijigeuze rimoti na kuanza kuwachezesha wanavyotaka. Usiruhusu ule ushauri wao wa mtu kutaka muishi kama anavyoishi yeye. Ishini nyinyi kama nyinyi. Kila mmoja wenu ameacha familia yake, mmekwenda kuanzisha familia mpya. Nyinyi ndiyo muwe madereva wa ndoa yenu. Muamue mnataka kuishi vipi. Hiyo ni taasisi yenu mmeianzisha, nyinyi ndiyo wakurugenzi. Hakuna mtu juu yenu atakayewapa amri ya kuishi.


 Nyinyi ndiyo mnapaswa kujitolea amri. Kabla sijamaliza barua yangu, nikupe jambo lingine la msingi sana katika maisha yako. Mtangulize Mungu mbele katika kila jambo. Yeye ndiye jibu la majaribu yote mtakayokutana nayo. 

Hakuna litakalowashinda endapo mtamkabidhi maisha yenu Mungu wetu wa mbinguni. Mkiwa na shida, muombeni yeye atawapa suluhu. Atafanya njia pasipokuwa na njia. Yeye ndiye njia ya kweli na uzima. Nikutakieni kila la kheri katika ukurasa mpya wa maisha mlioufungua, Mungu awabariki! Mimi ni kaka’ko;

Barua nzito na ERICK EVARIST  Maoni&Ushauri: 0768 811595

No comments