Header Ads

Irene Uwoya, Bhoke Wambura wamgombania Chid Benz!

TEMA nyongo! Ndivyo unavyoweza kusema. Mrembo ambaye hivi karibuni jina lake limeanza kutamba kwenye mitandao ya kijamii pia ni mtangazaji wa redio ya Jembe ni Jembe, Bhoke Wambura, amemtolea uvivu mwigizaji Irene Uwoya akidai amuachie mpenzi wake ambaye ni staa wa Bongo Fleva, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’.
 
 Bhoke alifunguka hayo hivi karibuni alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti hili na kubainisha kuwa anaumia kuona Uwoya anaingia kwenye anga zake wakati watu wa karibu na Chid wanamsema yeye kuwa aachane na Chid kwani anamrudisha kwenye matumizi ya madawa ya kulevya. 

“Nimeamua kuweka mambo hadharani kwa sababu kila kukicha Meneja wa Tip Top, Babu Tale ananisema kuwa nimemrudisha Chid kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kitu ambacho sio sahihi, mimi kwake nafuata mapenzi tu sasa nikisikia anaenda kwa Uwoya naumia maana mzigo nitakuwa nabebeshwa mimi kumbe pengine anayetakiwa kulaumiwa ni Uwoya,” alisema Bhoke. Akizidi kushusha ubuyu huo wa motomoto, Bhoke alisema kilichomfanya ashtukie mchongo, kuna siku alikuwa na msanii huyo kwenye gari, ghafl a Uwoya alimpigia simu Chid wakawa wanazungumza na kumuuliza kuwa atakwenda nyumbani kwake saa ngapi kitu ambacho kilimkera sana.

 “Jamani mtu niko naye njiani tumetoka kwenye raha zetu, ghafl a naona simu ya Chid inaita, kuangalia ni Uwoya na nilipomuuliza aliniambia ni mtu ambaye anamsaidiaga sana kumpa fedha na wakati mwingine huwa  anaenda kwake kukaa siku mbili mpaka tatu. “Kama mwanamke nilishindwa kumvumilia, tuligombana sana na Chid, aliniboa na huyo Uwoya nikamchukia pia. Nimemwambia Chid achague upande kati ya mimi au Uwoya, mimi namsikilizia,” alikuja juu Bhoke.

 Amani lilimtafuta Uwoya kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo ya Bhoke ambapo alipopatikana aling’aka kwa kusema anashangaa madai hayo kwani hata kwa hivi sasa hajui Chid yuko wapi na pia hadhani kama anapafahamu anapoishi na kamwe hawezi kutoa fedha yake hata siku moja kumpa Chid japokuwa walishawahi kuwa marafi ki sana huko nyuma. 

“Chid sidhani hata kama anapafahamu kwangu japokuwa alikuwa rafi ki yangu sana kitambo huko na pia mimi siwezi kutoa fedha kumpa Chid kwa sasa, hivyo itakuwa  wanadanganyana yeye na mpenzi wake maana hata sasa hivi sijui huyo mtu alipo,” alisema Uwoya. Alipotafutwa Chid ili kujua anazungumziaje madai hayo ya Bhoke, simu yake haikuwa hewani. Jitihada zinaendelea ili kumsikia kwa upande wake.

No comments