Header Ads

IRENE UWOYA: MAPEDESHEE SIKU HIZI HAWATOI PESA


MAMBO vipi mpenzi msomaji wa safu hii uipendayo ya 10 Question? Kama kawa, kama dawa wiki hii tunaye mwanamama ambaye bado ni mrembo, Irene Uwoya ‘Mama Krish’. Naye yuko hapa kujibu maswali mbalimbali ambayo amembana nayo na yeye akaonesha ushirikiano katika kuyajibu. Je, una shauku ya kujua ni maswali gani aliyobananishwa nayo na akajibu vipi? ‘Intaviu’ hii hapa chini inakuhusu… Ijumaa: Hivi ni ipi siri ya wewe kuonekana mrembo siku zote? Uwoya: Cha kwanza mimi najipenda sana, kingine napenda kutumia vitu kwenye ngozi yangu ambavyo havina madhara na nakula matunda sana.

 Ijumaa: Ni kweli wewe na Ndikumana bado ni mke na mume au ndo’ vile? Uwoya: Ndoa ya Kikristo haivunjiki bwana, mimi bado hakuna jinsi. Ijumaa: Hamna mpango wa kuishi pamoja na kumlea Krish wenu? Uwoya: Ipo siku Mungu atajaalia itakuwa hivyo. Ijumaa: Uliwahi kusema unataka kupata mtoto wa pili kupitia kwa huyohuyo Ndiku, hilo limefikia wapi? Uwoya: Niliwaza hivyo ila kwa sasa nimesitisha kwanza, kuna mambo inabidi nijipange kabla ya kuchukua uamuzi huo ni mkewe tu. Ijumaa: Sasa haoni wivu kukuacha mbali huku na yeye akiwa na maisha yake huko aliko?

Uwoya: Lazima atakuwa na wivu kwa mkewe lakini ndiyo hivyo tena
Ijumaa: Kuna madai kuwa umekuwa ukibadili vigogo, hilo unalizungumziaje? Uwoya: Unadhani ni rahisi sana wao kunipata? Yaani labda aje yule mkubwa wao (siwezi kumtaja). Ijumaa: Kuna wakati ilielezwa kuwa uliitwa na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata, ishu ilikuwa ni nini hasa? Uwoya: Kweli nilikwenda na kilichonipeleka kule siyo sahihi kukianika, jueni nilienda na nikarudi. Ijumaa: Soko la filamu ni kama limebuma hivi, sasa wewe unayaendeshaje maisha yako katika hali hiyo? Uwoya: Mambo ya filamu sasa hivi hayana nafasi kubwa kwenye maisha yangu, naendelea na vitu vingine kabisa kwani sasa hivi nina duka langu.

 Ijumaa: Kuna tetesi kwamba, kuna pedeshee mwenye nazo ndo’ kakushika sasa hivi na ndiye anayekupa jeuri ya kutofanya tena filamu, funguka mama. Uwoya: Hahaa! Hivi nani kakudanganya kuwa hao mapedeshee siku hizi wanatoa pesa za maana? Ijumaa: Inadaiwa kuwa wewe ni mkorofi sana na ndiyo maana hudumu na wapenzi, hilo lina ukweli? Uwoya: (Kicheko) siyo mkorofi, mimi ndivyo nilivyo halafu sitaki mwanaume anigande kiivyo. Ijumaa: Asikugande kivipi? Uwoya: Sitaki kwa sababu siyo ndugu yangu, ndiyo maana sidumu na wapenzi.

No comments