Header Ads

Jokate Asaka Msusi Bora Mkoa Wa Dar es salaamMwanamitindo, Jokate Mwigelo kupitia kampuni yake ya Kidoti ameandaa shindano la kusaka msusi bora alilolipa jina la Msusi Wao, lengo ni kuwaamsha wasusi wasiokuwa na ofisi na kuwafanya wakitambue kipaji chao.

Akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Escape One,  Jokate jana alisema kuwa alikaa na kuona kuwa kundi la wasusi ni watu muhimu  katika masuala ya urembo hivyo akaamua kuandaa shindano ambalo litawapa fursa ya kujiendeleza zaidi na kuitambua nafasi yao.

“Unajua siku moja nilitafuta msusi nikaletewa nyumbani dada mmoja ambaye hana ofisi  na ambaye alinisuka vizuri lakini nilipomhoji ana kazi gani inayompa kipato akasema hakuwa na kazi, ndipo niliona ipo haja ya kuwakuza wasusi wetu ikiwa sehemu ya kutoa ajira na kuwafanya wajitambue,” alisema Jokate.

Jokate alimtaja mshindi wa kwanza kuwa atapata nywele za Kidoti zenye gharama ya shilingi milioni 1.5 na pesa shilingi laki tatu na draya, wa pili atapata nywele za gharama ya shilingi milioni 1.2 na laki mbili na Draya na wa tatu atapata milioni moja na laki mbili na nusu pamoja na draya.

Washindi watatafutwa kila wilaya  ambapo kutakuwa na fomu za kujaza ili kuwatambua vyema na wanaohusika ni wale tu wasiokuwa na ofisi.

No comments