Header Ads

Jokate Asaka Msusi Bora Mkoa Wa Dar

Mwanamitindo, Jokate Mwigelo kupitia kampuni yake ya kidoti ameandaa shindano la kusaka msusi bora alilolipa jina la msusi wao lengo ni kuwaamsha wasusi wasiokuwa na ofisi na kuwafanya wakitambue kipaji chao.


Akiongea na waandishi wa Habari, Escape One Jokate jana alisema kuwa alikaa na kuona kuwa kundi la wasusi ni watu muhimu  katika masuala ya urembo ndio akaamua kuandaa shindano ambalo litawapa fursa ya kujiendeleza zaidi na kuitambua nafasi yao.


“Unajua siku moja nilitafuta msusi nikaletewa nyumbani dada mmoja ambaye hana ofisi ambaye alinisuka vizuri lakini nilipomuhoji anakazi gani inayompa kipato hakuwa na kazi, ndipo niliona ipo haja ya kuwakuza wasusi wetu ikiwa sehemu ya kutoa ajira na kuwafanya wajitambue,” alisema Jokate.


Jokate alimtaja mshindi wa kwanza kuwa atapata nywele za Kidoti zenye gharama ya shilingi milioni 1.5 Pesa shilingi laki tatu na Draya, wa pili atapata nywele za gharama ya shilingi milioni 1.2 na laki mbili na Draya na wa tatu atapata milioni moja na laki mbili na nusu pamoja na draya.


Washindi watatafutwa kila wilaya ya ambapo kutakuwa na fomu za kujaza ili kuwatambua vema na wanaohusika ni wale tu wasiokuwa na ofisi.

No comments