Header Ads

Kidoa na skendo ya kunusurika kubakwa maeneo ya Kinondoni jijini Dar

VIDEO Queen ambaye pia amejiingiza kwenye uigizaji wa filamu, Asha Salum ‘Kidoa,’ hivi karibuni aligandwa na madai ya kunusurika kubakwa ambapo inadaiwa tukio hilo lilimkumba maeneo ya Kinondoni jijini Dar.

 Asha Salum ‘Kidoa.
Chanzo cha habari kilichoomba kisitajwe jina lake kilidai kuwa, siku ya tukio maeneo ya Kinondoni Studio, saa 6 usiku alimsikia Kidoa akizozana na jamaa mmoja huku ikionekana kama waliokuwa wemezinguana.

 “Ninavyojua kile chumba wanaishi wanaume watatu na wamekuwa na tabia ya kuleta wasichana kisha kuwafanyia vitendo vibaya, sasa siku hiyo usiku kama saa 6 hivi nikasikia sauti ya msichana akilazimisha afunguliwe mlango atoke, kuchungulia hivi nikamuona ni Kidoa.

Inavyoonekana walitaka kumchangia ndipo likaibuka kasheshe,” kilidai chanzo hicho. Ili kupata ukweli wa habari hiyo, Ijumaa lilimpigia simu Kidoa na alipopokea na kuelezwa madai hayo alisema: “Ni kweli huwa naendaga pale Studio kwa kuwa kuna marafiki zangu lakini huyo anayedai nimesurika kubakwa atakuwa amenifananisha, kwanza nina muda mrefu sana sijaenda kule.”

No comments