Header Ads

Kim Kardashian atoboa siri ya kutompigia kura Donald Trump

WAKATI joto la uchaguzi mkuu wa rais Marekani unaotarajiwa kufanyika Novemba 8, mwaka huu likizidi kupamba moto, mwanadada mwenye jina kubwa duniani, ambaye pia ni mke wa Mwanamuziki Kanye West, Kim Kardashian amefunguka kuwa kura yake hawezi kumpa mwanasiasa anayewakilisha Chama cha Republican, Donald Trump kwa sababu si aina ya kiongozi ambaye dunia inamhitaji kwa sasa.

Kuhusu nani atampigia kura, Kim alisema baada ya kufanya uchunguzi wake kwa muda akiwafuatilia wanasiasa wote ambao wamejitokeza kuwania kiti cha urais na kupima sifa zao ikiwemo kusikiliza sera wanazozitoa,  amegundua kuwa Hillary Clinton ndiye mtu sahihi ambaye atampigia kura yake.

 “Linapokuja suala la kitaifa kama hili sihitaji kufikiria kuhusu mimi mwenyewe, nahitaji kuwaza kuhusu watoto wangu, matumizi mabovu ya silaha, kulinda haki za akina mama na maendeleo kwa ujumla ambapo nina uhakika basi la Hillary linanifaa sana kupanda,” alisema Kim. Hata hivyo, mbali na kauli hiyo, Kim na mumewe Kanye West wamewahi kuonekana kwenye mkutano wa Hillary Clinton uliofanyikia katika Ukumbi wa Scooter Braun’s Los Angeles Home, hapohapo Marekani jambo lililovifanya vyombo vya habari kuripoti kuwa wanamsapoti Hillary Clinton.

No comments