Header Ads

Lulu Diva adaiwa kujiuza Sauz

UNAIKUMBUKA ile skendo iliyowahi kumpata Video Queen Asha Salum ‘Kidoa’ ya kwenda kujiuza nchini Dubai? Kama jibu ni ndiyo, basi modo mwingine Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ naye hivi karibuni alitimkia nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ huku naye akidaiwa kuwa, kuna mwanaume alimlipia kila kitu ili aende kujiachia naye. Mtoa habari wetu ambaye ni rafiki wa karibu wa Lulu alisema: 
 
“Hivi unadhani Lulu atakuwa ameenda kufanya nini Sauz kama siyo kufuata madanga? Si unajua sasa hivi Sauz ndiyo kuna chimbo la mastaa kujiuza? Basi yeye kaenda, karudi wiki iliyopita na amesema siku si nyingi ataenda tena.” Ikazidi kuelezwa kuwa, anachokifanya Lulu ni kama kinachofanywa na mastaa wengine ambapo akitokea mtu akataka penzi kutoka kwa staa yeyote Bongo, wapo waunganishaji. 

“Kuna staa mmoja wa kike ambaye yeye ni kama dalali, akipata danga ‘mteja’, anakuunganisha, ukikubali anakukatia tiketi unakwenda kufanya yako kisha unarudi,” aliweka wazi mtoa habari huyo. 

Je, ni kweli Lulu alikwenda Sauzi kujiuza? Huyu hapa anatokwa na povu: ”Hicho ni kitu ambacho nilitarajia watu watasema, mimi nadhani ni wakati wa kila mtu kujali maisha yake, yaani mtu ukisafiri nje ya nchi tu, umefuata madanga, mh!”

No comments