Header Ads

Man Utd Yashinda dhidi ya Leicester City Bao 4-1, Pogba Atupia


man-utd-1
Juan Mata akifunga bao dakika ya 37 kipindi cha kwanza. Manchester Utd wameshinda bao 4-1 dhidi ya  Leicester City katika mchezo uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Old Trafford.
man-utd-2
Mata  akipongezwa na Rashford baada ya kufunga bao hilo.
man-utd-3
Beki wa Man United, Chriss Smalling (wa nne kushoto) akifunga bao kwa kichwa huku wachezaji wa Leicester wakijitahidi kuzuia bila mafanikio.man-utd-4
Nahodha wa Man United, Wayne Rooney (katikati) akiwa benchi na wachezaji wenzake.
man-utd-5
Zlatan Ibrahimovic (katikati) akipiga shuti mbele ya kipa wa Leicester lakini hata hivyo lilipaa.
man-utd-6
Marcus Rashford akifunga bao dakika ya 4o.
man-utd-8
Smalling akishangilia na Rashford.
man-utd-10
Wachezaji wa Manchester wakishangilia.
man-utd-11
Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic (kushoto) akicheka baada ya shabiki aliyefanana naye kuingia Uwanjani. 
man-utd-12
Paul Pogba akishangilia bao lake mbele ya mashabiki wa Man Utd.
man-utd-14
Rooney akipasha kabla ya mchezo kuanza, nyota huyu leo alianzia benchi ambapo aliingia kipindi cha pili.
man-utd-7
Kipa wa Man Utd, De Gea akishangilia ushindi wa timu yake.
man-utd-15
Makocha Claudio Ranieri na  Jose Mourinho (kulia) wakisalimiana.
 KIKOSI cha Manchester United leo kimerudisha furaha kwa mashabiki wake baada ya kupata ushindi wa mabao 4-1 mbele ya mabingwa watetezi wa Premier League, Leicester Cty.
United ambayo ilikuwa kwenye Uwanja wa nyumbani, Old Trafford ilionyesha soka safi hasa kipindi cha kwanza na kufanikiwa kuandika mabao yote manne huku nahodha wake, Rooney akianzia benchi.
Kwa matokeo haya, United inaongeza alama tatu na hivyo kufikisha jumla ya pointi 10 baada ya kushuka uwanjani mara sita ambapo wamefanikiwa kushinda michezo minne, imepoteza miwili na haijatoa sare.
Mabao ya United leo yalifungwa na: Smalling dakika ya 22; Mata (36), Rashford (39), Pogba (42) huku lile la Leicester likiwekwa kimiani na Gray dakika ya 60.
Manchester United: De Gea; Valencia, Bailly, Smalling (c), Blind; Ander Herrera, Pogba; Lingard (Carrick 78), Mata (Young 87), Rashford (Rooney 83); Ibrahimovic
Substitutes not used: Romero (GK); Rojo, Fosu-Mensah, Fellaini
Scorers: Smalling 22; Mata 36; Rashford 39; Pogba 42
Leicester City: Zieler; Simpson, Morgan (c), Huth, Fuchs; Mahrez (King 46), Amartey, Drinkwater, Albrighton (Schlupp 62); Vardy (Gray 46), Slimani
Substitutes not used: Hamer (GK); Hernandez, Okazaki, Ulloa
Scorer: Gray 60
Booked: Huth, Simpson
Referee: Mike Dean (Wirral) 

No comments