Header Ads

MASOGANGE ADAIWA KUWA NA NGOMA!Wameumbuka! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya wale ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakidai kuwa, video queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ana ngoma kwani mwanadada huyo amewaziba mdomo baada ya kwenda kupima na kukuta afya yake iko safi.
 
 Akizungumza mara baada ya kwenda kupima Ukimwi kimyakimya hivi karibuni, Masogange alisema kuwa, amekuwa akisikia watu wakieneza maneno hayo kuwa ana miwaya lakini kwa kuwa anayeijua afya yake ni yeye mwenyewe, amekuwa hajali na mara kadhaa amekuwa akienda kupima kama utaratibu wa kujihakiki afya yake.

Mwanadada huyo ambaye ni mmoja wa warembo maarufu Bongo waliojaaliwa kuwa na figa matata inayopambwa na lile kalio lake kiasi cha kuwadatisha wanaume wengi alisema, siku zote wanaokosa kazi za kufanya ndiyo ambao huzusha mambo wasiyo na uhakika nayo ili tu kuwaharibia wenzao.

“Nimekuwa nikisikia watu wakidai eti nina ngoma (Ugonjwa wa Ukimwi), wanaongeaongea tu na kwa kweli nimekuwa sitaki wanipotezee muda wangu. Nimekuwa nikiwapuuzia tu, kwa kuwa najua wamekosa kazi za kufanya,” alisema Masogange ambaye ni mama wa mtoto mmoja.

MADAI HAYO YAIBUA HOFU
Kufuatia kuenea kwa madai hayo, inadaiwa wapo baadhi ya wanaume ambao waliwahi ku-date (kutoka naye kimapenzi) ambao walianza kupata hofu wakidhani kuwa nao watakuwa wameambukizwa. Rafiki mmoja wa msanii wa filamu Bongo, Rammy Gallis ambaye anadaiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Masogange alilitonya gazeti hili kuwa, maneno ya chinichini
MARA

kwamba mpenzi wake huyo ‘anao’ yamekuwa yakimkosesha amani, lakini amekuwa akijipa moyo kuwa watu wanamzushia tu. “Unajua unaposikia mtu ambaye uko naye kwenye uhusiano watu wanadai ana ngoma, huwezi kuwa na amani na ndivyo ilivyokuwa kwa Rammy ila si unajua tena ukishapenda, unaziba masikio kuepuka maneno ya wambeya,” alisema rafiki huyo wa Rammy.

MASOGANGE AWAZIBA MIDOMO WAMBEYA
 Licha ya kwamba ni utaratibu wake wa kila wakati kucheki afya yake, hivi karibuni alikwenda kwenye hospitali moja kubwa jijini Dar (jina tunalihifadhi) na kupima Ukimwi na jambo la kushukuru likawa ni kwamba, alikutwa yuko HIV Negative, yaani hana! Ili kuwafanya wale wanaochonga sana juu ya afya yake wakose la kusema, ‘modo’ huyo aliamua kuyaanika majibu hayo ambayo gazeti hili liliyanasa na kubaini kuwa kilichokuwa kikivumishwa na watu hakikuwa na ukweli.

 AWAPOTEZEA WASHAKUNAKU Akizungumzia majibu hayo, Masogange alisema kuwa hakushangaa kukuta yuko safi kwani anajiamini na ndiyo maana alikuwa hayapi nafasi maneno ya washakunaku ambao amekuwa akiwapotezea.

No comments